Baada ya mahakama ya Mwanzo wilaya ya Nyamagana Mwanza kutupilia mbali pingamizi la usimamizi wa Mirathi ya Marehemu Askofu Moses Kulola,dhidi ya mchungaji Florian Katunzi,Siri nzito ya mvutano huo unaonendelea imebainika.
Mtoto wa pili wa kiume wa marehemu Askofu Kulola Bw.Willy Gabriel Kulola amesema kwamba wakati baba yake alizozidiwa na ugonjwa na ikalazimu asafirishwe kwenda India kulikua na upungufu wa Fedha kiasi cha shilingi Milioni 25,Zilizokaribia kumfanya ashindwe kwenda kutibiwa na wengi wa watoto wake hawakuonesha kumjali kiasi lakini mchungaji Katunzi alizitoa.Willy amesema kwamba Baba yake alikua akiishi nyumbani kwake Willy eneo la Chanika jijini Dar es Salaam,Karibu kipindi chote cha kuugua kwake na mtu aliyekua karibu nae na ambaye baba yake alipenda kumwita na kumuombea alikua na mchungaji Katunzi.
"Katunzi alikua kwenye Moyo wa Baba,ndio maana mimi sikushangaa baba alipomfanya kuwa mwanafamilia na kummwandikia wosia awe msimizi wake wa Mirathi""
Alisema Willy
Taarifa nyingine kama zilivyoripotiwa na gazeti la nyakati zinasema kuwa Siku Tisa kabla Askofu Kulola hajafariki akiwa katika hospitali ya Ami,jijini Dar es Salaam alimwekea mikono mchungaji Katunzi na kumtakia maneno mazito ya kumuachia wajibu wa uangalizi sio tu wa Familia ila pia wa kanisa la EAGT.
Mzee Kulola kama Nabii Eliya Hakufa kama mhuni ,aliacha Joho kwa Elisha wake,alisema mmoja wa wa watu waliokuwemo wakati wa tukio hilo huku akieleza kua siku hiyo chumba kilitawaliwa na vilio kwa waliokuwepo.
Hata hivyo hakutaka kuzungumzia kwa undani ikiwa hiyo inamaana kwamba mchungaji Katunzi ndiye ameachiwa Mafuta ya kuliongoza kanisa la EAGT ,Kwani Lina Utaratibu wake wa kikatiba usioongozwa na urithishaji utokanao na wosia wowote.
Katika mahojiano na Gazeti huru la Nyakati bwana Willy alipoulizwa alijibu hivi.
Mwandishi: Una nini cha kusema kuhusu hii migogoro inayoendelea kwenye Familia Yenu kuhusiana na mirathi ya baba yenu Askofu Kulola,unadhani kwanini mzee alimteua Mchungaji Katunzi kuwa msimamizi wa Mirathi yake??
Willy: Mungu ndiye aliyeongea na mzee ,kwa sababu hata ule wosia yeye (Mungu) ndie aliyemwambia afanye hivyo
Mwandishi: Ulijuaje kama Mungu alimwambia Mzee Kulola amteue mchungaji Katunzi?
Willy: Baba aliniambia Mwenyewe,maana alikua anakaa kwangu,na hawa wanaohoji ,Wanamhoji Mungu maana Katunzi hakuomba mwenyewe kuteuliwa ,Mungu alisema na Baba.
Mwandishi : Inaelezwa kua wewe ulikula njama na Katunzi kumhadaa Mzee kulola akamweka mwanao Mchungaji Michael ndiye awe mrithi wa Fungu la mama (mjane) huku ukijua utakua umepata wewe kwa mlango wa nyuma wewe unasemaje???
Willy: Hapana Hapana kabisa ,mbona mama yake Flora Mbasha alikuwepo pale na yeye pua ana watoto wakubwa kwanini kwanini yeye asiseme hapana,Nataka awe mtoto wangu, lazima nisema wazi Mzee kumteua katunzi ni mpango wa ki-Mungu utamuuliza nani??
Labda upige magoti umuulize Mungu akujibu.
Mwandishi : Lakini kwanini mnavutana kwa mali za kupita??
Willy: ndio maana mimi nasema ,tusiangalie mali ,tumuangalie mama yetu mjane kama hatutaki mjukuu arithi baada yake basi tumtunze mama aishi miaka 200.
Mwandishi : Una nini cha kuwaambia ndugu zako sasa?
Willy : Kwanza kabisa naomba watu wote watusamehe kwa hii aibu,hii mizozo inayoendelea ,maana mkizaliwa watoto wengi hamuwi wote wa aina moja,lakini hii mizozo inaumiza sana moyo wangu,kwa sababu hailingani na heshima aliyokua nayo baba katika utumishi wake,inaniumiza sana.
Mwandishi: Ndugu zako wanasema haiwezekani Katunzi Mhaya asimamie mirathi yao wasukuma,wewe unalionaje??
Willy: Kwanza msimamizi wa mirathi sio Mrithi ,Katunzi harithi chochote isitoshe alichoona mzee ndicho hicho baba hakua na mambo ya ukabila ndio maana aliweza kuhubiri injili nchi nzima.
wakati huohuo mjane ambaye ndiye aliyekua mke wa Askofu mkuu wa kanisa la EAGT marehemu Dr.Moses Kulola ,Bi.Elizabeth Kulola ameamua kufunguka na kumshutumu mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center, Florian Katunzi kua hana sifa za kua msimamizi wa Mirathi ya marehemu mume wake kwa sababu yeye si ndugu yao na hana sifa ya kuwasimamia .
Katika Shauri namba 109/2013 lililofunguliwa katika mahakama ya Mwanzo ya wilayani Nyamagana Jijini Mwanza,Mahakama ilitupilia mbali pingamizi la usimamizi wa Mirathi ambalo lilifunguliwa na baadhi ya watoto wa Marehemu Askofu Moses Kulola,waliokua wakipinga mchungaji Katunzi kuwa msimamizi wa Mirathi kama ilivyoagizwa na marehemu (mzee Kulola)
Katika Hukumu ya Kesi hiyo iliyosomwa Machi 4,2014 na Hakimu Ajala Mtani, alisema hoja zilizotolewa na upande uliokuwa ukipinga zilikua na chachu ya ukabila kwa kudai kuwa haiwezekani mhaya asimamie mirathi ya msukuma ambapo mahakama ilimuidhinisha rasmi Mchungaji Katunzi kuwa msimamizi rasmi wa mirathi ya Marehemu mzee Kulola.
Hakimu Mtani, alimuagiza mchungaji Katunzi kujaza fomu maalumu namba 5 na 6 na kisha kuiwasilisha katika mahakama hiyo April 5 mwaka huu,ikionesha mgawanyo wa mali za Marehemu kwa ajili ya hatua zaidi.
Watoto wa marehemu mzee Kulola wanaounga mkono wosia huo uliowasilishwa mahakamani na mchungaji Katunzi ni Willy Kulola,Carolina Kulola, na Anna Kulola, wanaoupinga ni pamoja na Mchungaji Daniel Kulola,Goodluck Kulola,Abel Kulola,Marry Kulola,Suzana kulola na Faith Kulola.
Katika mahojiano maalum na gazeti la Nyakati,watoto saba wa familia ya marehemu Askofu Moses Kulola,wakiongozwa na Mchungaji Dr.Daniel Kulola alidai kua kuna uvumi ambao umekua ukiandikwa kwenye vyombo vya Habari kua mchungaji Katunzi amepata ridhaa ya Mama Kulola (Mjane) kua msimamizi wa mirathi,Mahojiano hayo yalifanyika katika Hotel ya Colabus,Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
"Kabla sijamkabidhi Mama ,mimi ndiye kiongozi ambaye nawaongoza watoto Saba wa marehemu kua pamoja na kwamba tunaiheshimu Mahakama lakini Hukumu ambayo mahakama imeitoa haijatutendea haki na sisi kama familia hatujaridhika na uamuzi ule na tunaugazia umma kua tutakata Rufaa"
Alisema Mchungaji Dr.Daniel Kulola.
"Hebu shangaa Mzee ana wajukuu wengi iweje eti ampe mjukuu mmoja tu yaani mtoto wa Willy mali nyingi kuliko watoto wa kuzaa kama sio Willy alimrubuni mzee ni nini??
Katunzi sio ndugu yetu ,hatuhusu anaigawa familia ya mzee Kulola kwa maslahi Binafsi hivyo natangaza kua mimi siko upande wa Katunzi ,nipo Upande wa wanangu wanaopinga huo Wosia"
Mtoto mwingine wa Askofu Kulola Carolina ambaye ni mama wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Flora Mbasha amesema kua amekua akikerwa na kusumbuliwa na ndugu zake hao wanaopinga wosia wa baba yake kiasi ambacho amelazimika kuhamia mahali ambapo ni mama yake peke yake ndio anapajua
akiongea na mwandishi wa gazeti la Nyakati kwa njia ya Simu Carolina amesema kwamba kabla ya kukimbilia mafichoni,alipewa msukosuko kutoka kwa ndugu zake hao wanaopinga wosia huo ingawa mama yake alimwambia awapuuze.
Akimwongela mchungaji Katunzi Carolina amesema kua ndugu zake hawakumjali baba yao na mmoja wao alikua na pesa nyingi wakati baba yao akihitaji fedha za matibabu lakini alisema pesa zake zina majukum mengi,Lakini mchungaji Katunzi alisimamisha ujenzi wa kanisa akatoa kiasi cha shilingi Milion 25.
Carolina alisema ukarimu na ukaribu wa Mchungaji Katunzi kwa baba yao ndio uliomfanya amwone kuwa zaidi ya mwanawe wa kumzaa na kumpa kazi ya usimamizi wa mirathi.
"Baba aliniambia Nimemwandika kwenye Mirathi mtu mwenye msimamo ambaye atahakikisha mama yetu na nyie hampati tabu".
Watoto wangu hawajawa karibu nami katika shida hii,
alisema Carolina.
"Nikamuuliza ni nani huyo akasema bado ni fumbo mtajua nikishaondoka ndio baadae nikabaini kua ni mchungaji Katunzi".
Mtoto wa pili wa kiume wa marehemu Askofu Kulola Bw.Willy Gabriel Kulola amesema kwamba wakati baba yake alizozidiwa na ugonjwa na ikalazimu asafirishwe kwenda India kulikua na upungufu wa Fedha kiasi cha shilingi Milioni 25,Zilizokaribia kumfanya ashindwe kwenda kutibiwa na wengi wa watoto wake hawakuonesha kumjali kiasi lakini mchungaji Katunzi alizitoa.Willy amesema kwamba Baba yake alikua akiishi nyumbani kwake Willy eneo la Chanika jijini Dar es Salaam,Karibu kipindi chote cha kuugua kwake na mtu aliyekua karibu nae na ambaye baba yake alipenda kumwita na kumuombea alikua na mchungaji Katunzi.
"Katunzi alikua kwenye Moyo wa Baba,ndio maana mimi sikushangaa baba alipomfanya kuwa mwanafamilia na kummwandikia wosia awe msimizi wake wa Mirathi""
Alisema Willy
Mchungaji Florian Katunzi wa kanisa la EAGT City Center Dar es Salaam anayetajwa kua msimamizi wa mirathi ya Mzee Kulola |
Taarifa nyingine kama zilivyoripotiwa na gazeti la nyakati zinasema kuwa Siku Tisa kabla Askofu Kulola hajafariki akiwa katika hospitali ya Ami,jijini Dar es Salaam alimwekea mikono mchungaji Katunzi na kumtakia maneno mazito ya kumuachia wajibu wa uangalizi sio tu wa Familia ila pia wa kanisa la EAGT.
Mzee Kulola kama Nabii Eliya Hakufa kama mhuni ,aliacha Joho kwa Elisha wake,alisema mmoja wa wa watu waliokuwemo wakati wa tukio hilo huku akieleza kua siku hiyo chumba kilitawaliwa na vilio kwa waliokuwepo.
Askofu Dr.Moses Kulola enzi za uhai wake akiwa na mkewe Bi Elizabeth Kulola |
Mwandishi: Una nini cha kusema kuhusu hii migogoro inayoendelea kwenye Familia Yenu kuhusiana na mirathi ya baba yenu Askofu Kulola,unadhani kwanini mzee alimteua Mchungaji Katunzi kuwa msimamizi wa Mirathi yake??
Willy: Mungu ndiye aliyeongea na mzee ,kwa sababu hata ule wosia yeye (Mungu) ndie aliyemwambia afanye hivyo
Mwandishi: Ulijuaje kama Mungu alimwambia Mzee Kulola amteue mchungaji Katunzi?
Willy: Baba aliniambia Mwenyewe,maana alikua anakaa kwangu,na hawa wanaohoji ,Wanamhoji Mungu maana Katunzi hakuomba mwenyewe kuteuliwa ,Mungu alisema na Baba.
Mwandishi : Inaelezwa kua wewe ulikula njama na Katunzi kumhadaa Mzee kulola akamweka mwanao Mchungaji Michael ndiye awe mrithi wa Fungu la mama (mjane) huku ukijua utakua umepata wewe kwa mlango wa nyuma wewe unasemaje???
Willy: Hapana Hapana kabisa ,mbona mama yake Flora Mbasha alikuwepo pale na yeye pua ana watoto wakubwa kwanini kwanini yeye asiseme hapana,Nataka awe mtoto wangu, lazima nisema wazi Mzee kumteua katunzi ni mpango wa ki-Mungu utamuuliza nani??
Labda upige magoti umuulize Mungu akujibu.
Mwandishi : Lakini kwanini mnavutana kwa mali za kupita??
Willy: ndio maana mimi nasema ,tusiangalie mali ,tumuangalie mama yetu mjane kama hatutaki mjukuu arithi baada yake basi tumtunze mama aishi miaka 200.
Mwandishi : Una nini cha kuwaambia ndugu zako sasa?
Willy : Kwanza kabisa naomba watu wote watusamehe kwa hii aibu,hii mizozo inayoendelea ,maana mkizaliwa watoto wengi hamuwi wote wa aina moja,lakini hii mizozo inaumiza sana moyo wangu,kwa sababu hailingani na heshima aliyokua nayo baba katika utumishi wake,inaniumiza sana.
Mwandishi: Ndugu zako wanasema haiwezekani Katunzi Mhaya asimamie mirathi yao wasukuma,wewe unalionaje??
Willy: Kwanza msimamizi wa mirathi sio Mrithi ,Katunzi harithi chochote isitoshe alichoona mzee ndicho hicho baba hakua na mambo ya ukabila ndio maana aliweza kuhubiri injili nchi nzima.
wakati huohuo mjane ambaye ndiye aliyekua mke wa Askofu mkuu wa kanisa la EAGT marehemu Dr.Moses Kulola ,Bi.Elizabeth Kulola ameamua kufunguka na kumshutumu mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center, Florian Katunzi kua hana sifa za kua msimamizi wa Mirathi ya marehemu mume wake kwa sababu yeye si ndugu yao na hana sifa ya kuwasimamia .
Katika Shauri namba 109/2013 lililofunguliwa katika mahakama ya Mwanzo ya wilayani Nyamagana Jijini Mwanza,Mahakama ilitupilia mbali pingamizi la usimamizi wa Mirathi ambalo lilifunguliwa na baadhi ya watoto wa Marehemu Askofu Moses Kulola,waliokua wakipinga mchungaji Katunzi kuwa msimamizi wa Mirathi kama ilivyoagizwa na marehemu (mzee Kulola)
Katika Hukumu ya Kesi hiyo iliyosomwa Machi 4,2014 na Hakimu Ajala Mtani, alisema hoja zilizotolewa na upande uliokuwa ukipinga zilikua na chachu ya ukabila kwa kudai kuwa haiwezekani mhaya asimamie mirathi ya msukuma ambapo mahakama ilimuidhinisha rasmi Mchungaji Katunzi kuwa msimamizi rasmi wa mirathi ya Marehemu mzee Kulola.
Hakimu Mtani, alimuagiza mchungaji Katunzi kujaza fomu maalumu namba 5 na 6 na kisha kuiwasilisha katika mahakama hiyo April 5 mwaka huu,ikionesha mgawanyo wa mali za Marehemu kwa ajili ya hatua zaidi.
Watoto wa marehemu mzee Kulola wanaounga mkono wosia huo uliowasilishwa mahakamani na mchungaji Katunzi ni Willy Kulola,Carolina Kulola, na Anna Kulola, wanaoupinga ni pamoja na Mchungaji Daniel Kulola,Goodluck Kulola,Abel Kulola,Marry Kulola,Suzana kulola na Faith Kulola.
Marehemu Askofu Dr.Moses Kulola enzi za uhai wake akiwa na mwanae Mchungaji na mwinjilist Dr.Daniel Moses Kulola katika mkutano wa injili wa mwisho alioufanya katika kanisa la EAGT Lumala mpya mwaka 2012 |