Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuungana na kanisa la TAG Katika kusherehekea maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa nchini Tanzania,Maadhimisho yatakayofanyika jijini Mbeya katika uwanja Sokoine mnamo Julai 13,Mwaka huu 2014.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete |
Akielezea mbele ya waandishi wa Habari katika makao makuu ya kanisa hilo la TAG yaliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Barnabas Mtokambali amesema kuwa kanisa hilo kwa sasa linatimiza miaka 75 tangu lilipoanzishwa kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Igale jijini Mbeya ,rasmi mnamo mwaka 1939,
|
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Barnabas Mtokambali akifafanua jambo katika mkutano wake na waandishi wa Habari |
Mpaka hivi sasa kanisa hilo limefanikiwa kuwa na idadi ya waumini wapatao Milion 1 na laki 5 nchini Tanzania.
|
sehemu ya waandishi wa Habari waliokuwepo |
Aidha Askofu Mtokambali amebainisha kua Kanisa hilo la TAG ambalo kwa sasa limefanikiwa kua na makanisa yapatayo 7,000 nchi nzima limeanza maadhimisho haya ya miaka 75 mnamo mwezi January 18, 2014, ambapo yalizinduliwa rasmi na kuanza shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kiroho shughuli ambazo zimekua zikifanyika katika ngazi mbalimbali za kiuongozi katika kanisa hilo.
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho haya, miongoni mwa shughuli za Maendeleo ambazo kanisa hilo linatarajia kuzifanya kuanzia Julai 1 hadi 4 mwaka huu ni pamoja na huduma ya uchangiaji wa Damu, kugawa jumla ya Vyandarua takriban 8,200 vyenye thamani ya Shilingi Milion 300 katika jumla ya hospitali 34 na vituo vya afya 83 ikiwa ni vituo vya afya vya binafsi,Serikali, na hospitali zilizo chini ya taasisi za kidini bila kubagua dini yoyote,katika mikoa ya Rukwa,Mbeya,na Njombe.
|
Katibu mkuu wa kanisa la TAG Ron Swai akizungumza na waandishi wa Habari |
Hata hivyo Askofu Mtokambali ameeleza kua Kanisa la TAG limekua pia likijihusisha kikamilifu katika kushirikiana na jamii kukabiliana na kero na majanga mbali mbali ambayo yamekua yakijitokeza nchini ikiwa ni pamoja na njaa,Mafuriko pamoja na kutoa misaada mbalimbali magerezani na kwenye vituo vya watoto Yatima.
Askofu Mtokambali pia ameelezea mipango ya maendeleo ambayo kanisa hilo limejiwekea katika kuendana na ukomavu wa kanisa hilo kwa miaka 75 hivi sasa kua ni pamoja na kujenga shule za sekondari, za O-level na A-level, kujenga vyuo viwili vya ualimu mjini Tanangozi Iringa, na Himo Mjini Kilimanjaro.
miradi mingine ni pamoja na Chuo cha biashara mjini Bagamoyo na chuo cha Ufundi Veta kinachotarajiwa kujengwa huko Lindi.
Katika sherehe hizo za Maadhimisho ya miaka 75 ya jubilee kwa kanisa hilo la TAG pia zitaambana na dhifa ya kitaifa kwa kuhusisha wamishenari wote waliowahi kuhudumu hapa nchini kupitia kanisa hilo,Kongamano la wachungaji wapatao 6000 kutoka mikoa yote nchini Tanzania pamoja na mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika jijini Mbeya na kuwahubiria watu wote habari njema za ufalme wa Mungu.
Picha zaidi za mkutano huo alioufanya Askofu mkuu Mtokambali na waandishi wa Habari ni kama zinavyoonekana hapa chini.
Picha kwa hisani ya Rulea Sanga