Hatimaye Taarifa zilizotufikia kutoka chanzo kimoja wapo cha Habari zinasema kua Mchungaji Daniel Mwasumbi wa kanisa la EAGT ameachiwa huru na Mahakama kuu baada ya awali kesi yake alihukumiwa kifungo cha Maisha Jela baada ya kuhukumiwa na mahakama kwa makosa yaliyotajwa kua ni ya Ubakaji.
kupitia kwenye account ya Facebook ya matoto wa mchungaji huyo,Gamaliel Mwasumbi ameandika ujumbe huu
Niwashukuru Marafiki zangu wote waliohusika kwenye swala zima la Baba yangu Rev DANIEL MWASUMBI bila unafiki.Napenda kuwajulisha Mzee wangu Mtumishi wa MUNGU MWASUMBI MAHAKAMA KUU IMEMUACHIA HUKU KWA KESI YA UBAKAJI ALIYOkUWA AMEBAMBIKIZIWA NA BAADHI YA WACHUNGAJI WENZAKE NA MAASKOFU WA EAGT KWA MASLAHI BINAFSI.Ungana nami Kwa niaba ya familia ya Rev Daniel Mwasumbi kumshukuru JEHOVAH amefanya!
Huku chanzo kingine kikiwa Radio Ushindi FM 98.6 ya kutoka Mbeya wao wameripoti kua
MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA LEO JUNE 03 IMEBATILISHA HUKUMU YA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA WILAYA MBEYA DISEMBA MWAKA 2013 DHIDI YA MCHUNGAJI DK.DANIEL MWASUMBI ALIESHTAKIWA KWA MADAI YA KOSA LA UBAKAJI...
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA MBEYA IMEMSAFISHA MCHUNGAJI MWASUMBI KWA KUIBUA HOJA ZA KISHERIA ZAIDI YA NNE ZILIZOBAINISHA KUWA HUKUMU ILIYOTOLEWA DHIDI YA MCHUNGAJI HAIKUWA SAHIHI
Awali Mchungaji huyo mwaka jana mwezi July 2013, habari ambayo iliibua ukakasi kwenye vichwa vya watu wengi ilikua inasomeka kama ifuatavyo
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.