Mtakapo kujua juu ya siha yangu, mimi ni bhuheri wa afya; hofu na mashaka ni kwenu mlio mbali na upeo wa mboni za macho yangu.
Mwandishi James Kalekwa |
Ama baada ya salaam, ni kwa muda sasa nimekuwa nikitafuta namna ya kuwafikia na kuwaelezeni yaujazayo moyo wangu…
Siku moja, nikiwa nimepumzika nyumbani kwa wazazi wangu (nikiwa nasubiri kupata ajira baada ya kuhitimu masomo yangu), nikifuatilia maswaala ya ubunifu ndipo nikapata fursa ya kutazama kazi za mpuuzi mmoja aitwaye Masoud Kipanya (ni moja ya wapuuzi niwapendao) na namshukuru Mola kwamba ndugu huyu alijifahamu kuwa ni mpuuzi hivyo kazi yake kuiita “UPUUZI WA MASOUD KIPANYA.” Nakushauri ujisumbue kuutafuta upuuzi huo!
Mpuuzi Masoud Kipanya analeta nadharia ya vipande 26 vya keki na jinsi gani vinagawanywa kwa watu waliopaswa kuvipata.
Kuna watu 26 mahali fulani na kutoka “kusikojulikana” wanakuja waokaji na kuwatengea watu hao sinia kubwa la keki… mbele ya msosi akili hufyatuka! Watu hao wakaishiwa ustaarabu kwa ghafla na kuanza kukuru kakara za kugombania kupata kubugia keki hiyo.

Wapendwa walimwengu, salaam nyingi za upendo kutoka kwa mtumwa!
Hawakujua kuwa wanatumia nguvu zao nyingi sana kupigana na kuumizana badala ya kushirikiana na kusaidiana ni kwa namna gani wote kwa pamoja wanaweza kunufaika na keki hiyo.
Lakini ghafla wanaibuka watu watatu kutoka miongoni mwao wanaoona (Nimesema wanaoona si wanaotazama) kuna hitaji la kutengeneza utaratibu mzuri wa kugawana keki.
“Jamani, kuna maana gani kuendelea kugombana wakati twaweza kuwa na namna nzuri kufaidi keki yetu na ukizingatia ni kwaajili yetu sote…” .
Watu woote wakafurahia wazo la wenzao watatu. Waliotoa wazo hujua namna ya kulitekeleza, basi hatua ya kwanza ilikuwa ni kupata idadi kamili ya watu ili kujua ni kwa kiasi gani kila mmoja anaweza kufaidi keki yao.
Loh! Ajabu na kweli, idadi ya watu ilikuwa ni 26 (pamoja na wale ndugu watatu) ilihali vipande vya keki vilikuwa 26; Hivyo basi kila mtu alikuwa na kipande kimoja ndani ya sinia… “Kwanini tulikuwa tunapigana jamani…???”

kila mmoja alijiuliza moyoni mwake. “Utaratibu ni kwamba woooote tutajipanga foleni kuja kupokea kipande cha keki” alisikika mmoja wa jamaa watatu akitoa maelezo, wakati huo yeye na wenzake wamechukua dhamana na jukumu la kuwa wagawaji wa keki hivyo wamesimama nafasi ya mbele….
Nilisema hapo awali msosi huwafanya watu warukwe na akili….
Watu walianza kukimbizana tena kuwahi nafasi kwenye foleni ili kila mmoja apate kwanza! Wakati natazama upuuzi wa Masoud ghafla wazo likaniijia “Kama kila mtu anataka kupata kwanza, nani atakuwa wa mwisho tena nikakumbuka kuwa huwezi kuitwa wa kwanza kama hakuna wa pili, wa tatu na wa “mwisho”…”
Nikagundua kumbe walikuwa wanapigania “kitu kisichokuwepo”…. Kweli nilicheka kwa huzuni!
Hatimaye utaratibu ukatolewa kwamba kwakuwa kila mtu ana nafasi sawa ya kupata kipande kimoja, basi uwepo utu na kuwaachia nafasi na kuwatanguliza wanawake wajawazito, walemavu, watoto, wazee na vikongwe na wale wenye uwezo wa kuvumilia watapata baada ya hao.

Ikampendeza kila mmoja na kuafikiwa hivyo. Wale jamaa watatu wakaona kwa kuwa na wao ni sehemu ya wale watu 26, hivyo hakuna ubaya kama na wao watajigawia vipande vyao; kimoja kwa kila mmoja. Moyoni mwa mtu mbali! Jamaa wawili kati ya wale watatu walikuwa na tamaa…
Wakaamua kuchukua vipande vitatu yaani kimoja kilichokuwa haki ya kila mmoja na viwili vya ziada kwa kila mmoja wao.
Foleni ikasogea, na watu wanne wa mwisho wakakuta sinia tupu (keki zao zilikuwa mikononi mwa jamaa wawili wenye tamaa)…. Kilichofuata hapo waweza kukiona ndani ya upuuzi wa mpuuzi Masoud! (Nimesimulia kwa maneno yangu)
Wahenga walisema “Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba!” nami nasema inahitaji mpuuzi kumwelewa mpuuzi mwenzake… nilimwelewa Masoud.
Wapendwa niwapendao walimwengu, ninapenda kutumia fursa hii adhama kueleza kwa maneno rahisi sana juu ya wale jamaa watatu waliokuwa wakigawa vipande vya keki na wengine wengi wanaofanana na hao hivi leo…

Napenda kuzungumza juu ya viongozi na uongozi na hatma ya ulimwengu (Tanzania ni sehemu ya ulimwengu)!
Watoto wadogo wa miaka mitano au chini ya hapo, wanapokutana katika michezo yao hutokeza mtoto mmoja ambaye husikilizwa na wenzake naye hutoa mwelekeo wa namna gani wacheze. Kwenye timu ya mpira kuna utaratibu ambao mtu mmoja huwaongoza wanatimu wenzake.

Kwenye tasnia na filamu vivyo hivyo na kwenye familia zetu huwapo mtu ambaye hutoa mwelekeo ndivyo ilivyo kwenye taasisi za elimu, nyumba za ibada hata kwenye kijiwe cha kahawa…
Kiongozi ni mtu muhimu sana na kwa picha kubwa ya namna hiyo ni dhahiri kwamba jamii husika haiwezi kufikia hatma yake kwa mafanikio pasi na kiongozi.
Watu wengi wamejikita kuzungumza namna ya kumpata kiongozi (ninakiri kwamba kuna namna nyingi za kuwapata viongozi) lakini kabla ya kwenda huko kwenye namna ni hekima iwapo tutawekeza muda wetu kujua kiongozi ni nani… Kimsingi nataka kujenga hoja juu ya tabia za ndani za kiongozi!
Historia inaeleza ni kwa jinsi gani nchi ya China ya kale (Ancient China) ilivyochoshwa na uvamizi wa genge la wavamizi toka Kaskazini hivyo wakanuia kwa pamoja kutafuta namna ya kujiweka salama; walijenga Ukuta Mkuu wa China “The Great Wall of China”.

Ulikuwa ni ukuta mrefu sana kiasi kwamba hakuna adui angeweza kuupanda na ulikuwa ni mpana sana kiasi kwamba hakuna kitu kingeweza kuuangusha.
Wachina wa kale wakaendelea kuishi wakiufurahia usalama, amani na utulivu ulioletwa na ukuta huo. Miaka mia moja ya kwanza ya uwepo wa ukuta huo, China ya kale ilivamiwa mara tatu na chakushangaza, wavamizi hawakuupanda wala kuuvunja ukuta.
Historia inatueleza kwamba wavamizi waliwahonga walinzi wa lango kuu nao walinzi waliwafungulia wavamizi hivyo uvamizi ukafanyika kiulaini kiasi hicho kupitia kwenye lango kuu (geti).
Unajua hawa wachina wa kale walijibidiisha kuweka tumaini lao kwenye ukuta mkuu kiasi kwamba hawakujisumbua kutafuta mlinzi/walinzi mwenye uadilifu/unyoofu!