Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini Lundi Tyamara (38) amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Edenvale alipokua akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa TB ya tumbo na ugonjwa wa Ini.
Kituo cha Televisheni cha One Gospel kimeripoti.
Mkali huyu anayetamba na kibao cha Ndixolele imeelezwa kuwa Jumatatu ya wiki hii alikimbizwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafla na kuwekwa katika wodi ya uangalizi maalum 'ICU' huku chanzo cha kuaminika cha taarifa kikisema kuwa mwanamuziki huyu baada ya kufikishwa hospitalini aliwekewa mipira kwa ajili ya kumsaidia kupumua 'oxygen' baada ya kubainika ini mwilini mwake kuacha kufanya kazi.
Lundi alilazwa hospitali mwishoni mwa Disemba mwaka 2016 baada ya kurudi kutoka China alipokua ameenda kwa ziara.
Familia ya Lundi imetoa taarifa fupi ikithibisha kuhusu kifo chake na kusema Lundi amefarikia usikua wa kuamkia leo katika hospitali ya Edenvale Johannesburg alipokua anapatiwa matibabu.
Mwanamuziki Lundi Tyamara enzi za uhai wake
Kituo cha Televisheni cha One Gospel kimeripoti.
Mwanamuziki Lundi Tyamara |