Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania Paul Clement amezindua Video yake mpya ya wimbo unaokwenda kwa jina la 'Amenifanyia amani' uzinduzi uliofanyika jijini Dar siku ya ijumaa October 7, 2016 .
Video hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Fishers chini ya Director Geofrey inatarajiwa kuanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni na katika mitandao ya kijamii kuanzia sasa.
Akifafanua katika uzinduzi huo Kiongozi wa kampuni hiyo ya Fishers Mr.Geofrey alisema kua wanataka kufanya mapinduzi katika muziki wa injili nchini kwa kutoa kazi za video zenye ubora wa kiwango cha juu na kuweza kuukuza mziki wa injili kuweza kufika ngazi za kimataifa na sasa wameanza na Paul maana wanaamini ana kitu ndani yake cha kipekee kihuduma.
Awali kabla ya uzinduz wadau mbalimbali walipata fursa ya kuzungumza kuhusu mziki wa injili Tanzania na maendeleo yake ambapo Muandaaji wa matamasha ya muziki wa injili Prosper Mwakitalima alielezea namna wanamuziki wa injili wanapaswa kujitambua thamani yao "Brand'' na kujiongeza thamani katika kazi wanazozifanya ili waweze kufika mbali wakiwa na ubora badala ya kufanya muziki kwa mazoea.
Msemaji mwingine alikua Fred Msungu ambaye alielezea namna mwanamuziki wa injili akijitambua yeye ni nani na nini anapaswa kukifanya ili mziki wake ufike mbali anaweza kujipatia matokeo makubwa kuanzia kiuchumi na hata kihuduma.
Katika kuhitimisha Mzungumzaji wa mwisho alikua ni Jimmy Temu Mtangazaji wa kipindi cha Chomoza cha Clouds Tv ambapo aliwataka wanamuziki wa Injili nchini kubadilika na kuanza kutoa video zenye ubora ili ziweze kumudu ushindani uliopo katika video zenye ubora sokoni na pia ili ziweze kupata nafasi ya kuchezwa kwenye TV mbalimbali
"Changamoto iliyopo kwa sasa ni kwamba unakuta video inakuja mtu anataka uicheze kw TV lakini sasa video ina quality mbovu ambapo ukiingiza katika system ili ichezwe hewani kwa Tv, quality yake inashuka,,, wanamuziki wa injili inabidi sasa wabadilike kwani hawa wa Bongo flava kwanini watuzidi ilhali sisi tuna Mungu afadhali Angel Benard sasa video yake imeanza kuonesha njia na tunaweza kusimama kifua mbele kwamba na sisi tunaweza kutoa video zenye ubora", alisema Jimmy
Katika uzinduzi huo ambao uliohudhuriwa na wadau mbalimbali na waimbaji wa muziki wa injili nchini, Paul Clement amesema anamshukuru Mungu kwa kuweza kufanikisha Video hii ambapo anaamini haitaishia tu kuwa video au wimbo bali itakua kama pambio ya ushuhuda kwa wengi kumshukuru Mungu kwa mambo anayowatendea kwa kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine.