Waziri mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu Fredrick Tluway Sumaye amezindua kitabu kipya kabisa kiitwacho Kufurahia ndoa ambacho kimeandikwa na mchungaji Zakayo na Carol Nzogere wachungaji wa kanisa la Mwanza International Community Church katika uzinduzi uliofanyika siku ya jumapili hii na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji la Mwanza.
Katika kuzindua kitabu hicho Mh.Sumaye ameelezea kua Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa waandishi wa vitabu kama mchungaji Zakayo na Carol Nzogere na waandishi wengine wengi zaidi ambao watafanyika kua chachu ya maendeleo na kutatua matatizo mengi kupitia kuyaweka mawazo yao katika maandishi picha au kumbukumbu ya kile kilichowahi kuwatokea ili yaweze kuwasaidia na kutoa manufaa kwa watu wengine watakaosoma mawazo hayo katika vitabu.
Aidha Sumaye amewapongeza Mchungaji Zakayo na Carol Nzogere kwa kuweza kutumia muda wao na maarifa yao katika kuandika kitabu hiki ambacho kinaeleza wanandoa wafanye nini ili ndoa zao zipate kuwa imara na pia kuweza kutatua tatizo linalokua siku hadi siku hadi siku katika taifa, tatizo la ndoa nyingi kutetereka hadi kuvunjika na kupelekea kutokea kwa matatizo kama chuki baina ya waliokua wana ndoa, maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa wanandoa pale ambapo wanandoa huanza kukomoana kwa kuanza michepuko nje ya ndoa.
Aidha Sumaye ameeleza migogoro mingi ya ndoa imepelekea uchumi wa wanandoa kuvurugika na kupelekea ongezeko la watoto yatima na watoto wa mitaani ikiwa ni pamoja na kukosa huduma muhimu kama elimu,afya bora na malezi ya baba na mama.
Kufuhia ndoa ni kitabu ambacho kimeandikwa na Mchungaji Zakayo na Carol Nzogere, wachungaji na wanandoa ambao wamepata kudumu katika ndoa yao kwa miaka 14 sasa ,kitabu ambacho kimebeba maudhui ya masuala ya ndoa kwa ujumla kikiwa na mafundisho juu ya namna ya kuiboresha ndoa kwa watu waliopo ndani ya ndoa na wengine ambao wapo katika mchakato wa kufunga ndoa hivi karibuni ili waweze kupata maarifa namna gani ya kuzifanya ndoa zao ziwe zenye furaha na amani tele katika maisha yao yote.
Akisoma taarifa fupi kuhusu kitabu hicho Mchungaji Zakayo emeeleza kua dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la ndoa ambalo limekua chanzo cha matatizo mengine ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa watoto wa mitaani.
Unzinduzi huo wa kitabu hiki cha Kufurahia ndoa pia ulihudhuriwa na Maaskofu wa makanisa ya kipentekoste na wachungaji mbalimbali wa jiji la Mwanza na baadae wakapata fursa ya kuweka mikono na kukibariki kitabu hicho kwa njia ya maombi kwa ajili ya wote watakaopata nafasi ya kukisoma kitabu hicho wakapate kubarikiwa na kufunguliwa kwa wote wenye migogoro ya ndoa zao.
Picha zaidi za uzinduzi huo ni kama zinavyoonekana hapa chini.
waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akikiangalia kitabu cha Kufunurahia ndoa,kulia ni mchungaji Zakayo na Carol Nzogere wakifatilia kwa umakini |
mh.Sumaye akikata utepe na kukizindua rasmi kitabu hicho cha Kufurahia ndoa |
Watunzi na waandishi wa kitabu cha Kufurahia ndoa Mchungaji Zakayo Nzogere na Carol Nzogere wa kanisa la Mwanza international Community church MICC |
Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Mh Fredrick Tluway Sumaye akitoa hotuba yake |
Mchungaji Zakayo Nzogere wa kanisa la MICC akitoa hotuba kuhusu kitabu cha Kufurahia ndoa |
Mchungaji Zakayo na Carol Nzogere wakapata fursa ya kuimba wimbo waliouimba siku ya harusi yao miaka 14 iliyopita |