Mheshimiwa Samwel John Sitta ameshinda katika uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba, ambapo amemshinda mpinzani wake pekee katika nafasi hiyo mheshimiwa Hashim Rungwe.
Kinyang'anyiro hicho kimemalizika hivi punde na kumpa nafasi Mh Sitta kuliongoza bunge hilo la kihistoria kwa Tanzania katika kuandika Katiba mpya ya Tanzania
Katika uchaguzi huo uliofanyika majira ya jioni mjini Dodoma ,ndani ya ukumbi wa Bunge , jumla ya kura zilizopigwa ni 567 ambapo jumla ya Kura zilizoharibika ni 7
Mgombea pekee katika kinyang'anyiro hicho cha kumtafuta Spika /Mwenyekiti wa Bunge hilo maalum la Katiba ,Hashimu Rungwe amepata kura 69 ambazo ni sawa na 12.3% na Samuel Sitta amepata kura 487 na kumfanya kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa bunge la Katiba.
Kinyang'anyiro hicho kimemalizika hivi punde na kumpa nafasi Mh Sitta kuliongoza bunge hilo la kihistoria kwa Tanzania katika kuandika Katiba mpya ya Tanzania
Mheshimiwa Samwel John Sitta |
Mgombea pekee katika kinyang'anyiro hicho cha kumtafuta Spika /Mwenyekiti wa Bunge hilo maalum la Katiba ,Hashimu Rungwe amepata kura 69 ambazo ni sawa na 12.3% na Samuel Sitta amepata kura 487 na kumfanya kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa bunge la Katiba.
Wajumbe wakipiga kura |
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo |
Aliekuwa Mgombea Mwenza wa Nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Hashim Rungwe akizungumza machache mara baada ya kukubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika Bungeni hapo uliompa Ushindi wa Nafasi ya Uenyekiti,Mh. Samuel Sitta kwa kura 487. |
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Edward Lowassa na Mh. Anne Tibaijuka wakibadilishana mawazo wakati Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge hilo ukiendelea. |
Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Samuel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Bunge hilo,Mh. Paul Makonda. |
Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Samuel Sitta akipongezwa na Wajumbe mbali mbali wa Bunge hilo. |