Kiongozi wa zamani wa kundi la kusifu na kuabudu toka kundi la Hillsongs la nchini Australia hatimaye amemaliza sehemu ya tano ya matibabu (Chemotherapy) katika muendelezo wa matibabu ya tatizo la Saratani (Cancer ya titi)linalomkabili .
Mnamo December 29,2013 Mwanamuziki huyu aliandika kwenye blog yake kuwa baada ya kufanyika vipimo ilibainika kua alikua na tatizo la saratani ya titi na tangu kipindi hicho amekua akiendelea na vipimo na matibabu mbalimbali.
Katika moja ya kauli alizozitoa mwanamuziki huyo alisema kua
"To be completely honest, this is not the kind of news anyone ever really wants to tell. However, I have seen two absolute miracles in my body thus far and I know there will be many more to come," alisema Darlene na kunukuu kitabu cha biblia Warumi 5:3-5 akisema
"Not only so, but we also glory in our sufferings, because we know that suffering produces perseverance, perseverance character and character HOPE. And hope does not put us to shame, because God's love has been poured out into our hearts through the Holy Spirit, who has been given to us."
Zschech amekua mtu maarufu sana duniani katika huduma ya mziki wa Gospel kutokana na aina ya huduma ya uimbaji ambayo ameifanya kwa mda mrefu ikiwemo utunzi wa nyimbo za kuabudu ikiwa ni pamoja na wimbo ujulikanao kama "Shout to the Lord."
Baada ya kuhudumu kwa muda mrefu kama mchungaji na kiongozi wa sifa na kuabudu katika kanisa la Kipentecoste la Hillsongs nchini Australia kwa zaidi ya miaka 10, baadae alitoka na kwenda kuanzisha kanisa lingine yeye na mume wake aitwaye Mark.
kwa pamoja wamekua wakiongoza katika kanisa la Hope Unlimited Church huko Central Coast of New South Wales tangu mwaka 2011.
Habari zinazidi kutanabaisha kua tangu kutangazwa Zschech amekua akiandika kuhusu safari yake hiyo ya matibabu na kupata nguvu kutokana na maombi ambayo amekua akiombewa na watumishi wa Mungu mbalimbali kipindi hiki cha miezi 6 ya matibabu yake.
Moja ya kauli zake Darlene Zchech amesema: "I am assured of God's love for me. Truly this has been one of the sweetest parts of the journey. My beautiful Emmanuel is never far away. Our Friends, family and our beloved church family are amazing every day. I'm ever convinced that life was always designed to be done in true community. Good days and bad days yet always better together."
na hapa anasema
"In fact, we are already planning a Thanksgiving service at our church in November, where we will record songs birthed during this season. We simply want to fill the place with praise for all that God has done," she added.