Mhubiri mmoja huko Afrika kusini ambaye amefahamika kama Pastor Lesego Daniel wa kanisa lililofahamika kama Rabboni Centre Ministries mapema wiki hii ameripotiwa kuwapa amri waumini wake kula majani au nyasi mabichi kama moja ya masharti ya waumini wake kuwa karibu na Mungu kwa kula majani kama vile wanyama aina ya kondoo au mbuzi ambao chakula chao ni majani au nyasi. huku akiwaambia kua binadamu ameumbiwa kula chochote kile.
Baada ya waumini hao kula majani hayo baada ya mda kupita waumini hao walijikuta wakiwa katika hali ya mkimbizano kila mmoja akijikuta akitatapika na wengine kuvutana kwenye vyoo ikiwa ni katika kuwahi kujisitiri baada ya kukumbwa na mchafuko wa tumbo la kuhara uliowakumba ghafla baada ya kula majani hayo![]() |
huyu ndiye mchungaji Lesego Danielaliyewaagiza waumini hao kula majani |



Baada ya waumini hao kula majani baada ya mda mfupi walianza kuugua ghafla na wengine kujikuta wakitapika na kushikwa na homa ya matumbo na hali ilikua kama inavyoonekana katika picha hapa chini.


