Mahakama kuu Zanzibar mapema leo hii imemuachia kwa dhamana Omari Musa Makame ambaye ni mtuhumiwa katika kesi ya Mauaji ya Padre Mushi aliyeuwawa February 17 mwaka huu 2013 huko Zanzibar kwa kupigwa Risasi wakati akielekea kwenye Ibada siku ya jumapili
katika Dhamani hiyo iliyotolewa leo hii wadhamini wawili wamesaini mahakamani na kutoa dhamana ya pesa taslim kiasi cha Laki 5 kila mmoja
Padre Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar na mtuhumiwa alitiwa mbaroni na Polisi tangu Machi 17 mwaka huu.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Omar Mussa Makame (35) aliyevaa shati la rangi ya waridi akiwa Mahakamni |