Shetani analeta wazo la dhambi kwenye fikra zako; ukilipokea na kulitendea kazi hiyo ndo dhambi, bali ukilipinga na kutolipa nafasi, umeshinda; uamuzi wa kutenda au kutotenda dhambi ni wako, na mungu atakuhesabia haki au kukuhukumu kwa maamuzi yako hayo (soma hapa zaidi)!
Anania na safira mkewe katika kitabu cha matendo 5 ni mfano halisi wa kile ambacho nakizungumzia hapa.
Anania na mkewe "walikufa kwa kosa la kumwambia uongo roho mtakatifu" (mst 3), lakini "huo uongo" anania na mkewe safira "waliingiziwa ndani ya mawazo yao na shetani", na ndiyo maana petro anasema, "kwanini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo roho mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?" (mst 3)
kosa la anania na mkewe si "kuzuia sehemu ya thamani ya kiwanja" bali kosa lao ni "kumpa ibilisi nafasi" ya "kuwasemesha wapunguze sadaka waliyopanga kumtolea mungu"... Kama anania na mkewe safira "wangelimpinga shetani; hakika angeliwakimbia" (yakobo 4:7)... Kosa lao lilikuwa "kukubali kupokea lile wazo lililo kinyume na kisha kuanza kuliwaza mioyoni mwao na kisha kulitendea kazi"
ndivyo ilivyo kwako pia:
dhambi zote ulizowahi kutenda, "zilikuja kwenye mawazo yako hapo kwanza kama wazo" halafu "ulipokubali kulipokea na kuliwaza" ndipo "ulipoishia kulitendea kazi"
kaka "uliona mguu, paja, maziwa au kiuno cha dada fulani" halafu ghafla "shetani akakuletea wazo ndani yako kwamba unaonaje ukiwa naye kitandani huyu?" halafu wewe badala ya "kulipinga kwa jina la yesu na kulifuta kwa damu ya yesu" wewe ukaamua "kuendelea kulitafakari, likahama toka kwenye kichwa chako, likaja moyoni, moyoni likasambaa mwili mzima pamoja na damu yako, na mwisho wa siku ukaishia kutenda dhambi"
kosa lako ni "kulifuga wazo lile hasi, wazo la dhambi" ulipaswa "kulipinga kama ambavyo unaweza kumpinga shetani mwenyewe" maana "shetani hatakuja kwako waziwazi lakini atakuletea mawazo yake maovu" na wewe "ukiyapinga na kuyafuta kwa damu ya yesu utakuwa salama" lakini "ukikosea na kuyapa nafasi ya kuyawaza na kuyatafakari, hakika utaishia kutenda dhambi"
biblia inatuambia cha kufanya:
"wala msimpe ibilisi nafasi" (waefeso 4:27).
Ukifanya kosa kuruhusu "wazo hasi; wazo la dhambi kuendelea kubaki kichwani mwako; litahamia moyoni, na litasambaa kwenye mwili wako na utaishia kutenda dhambi"
"tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo" (2wakorintho 10:5)
wewe ndo unayewajibika "kuangusha mawazo" yote ambayo "ndani yake yamebeba dhambi na uasi dhidi ya mungu na neno lake"
wewe ndo unayewajibika "kuteka kila fikra mbovu, ya dhambi na uasi" kwa mamlaka ya "jina la yesu na damu yake" ili mwisho wa siku ubakize "mawazo na fikira zinazokubaliana na utakatifu, neno la mungu na mapenzi ya mungu"
"basi mtiini mungu. Mpingeni shetani naye atawakimbia" (yakobo 4:7).
Wewe ndo unayewajibika "kumpinga shetani" aliyekujia kwa njia ya "mawazo na fikira za uovu", wewe usipochukua hatua ya "kumpinga shetani na mawazo yake" badala yake "ukayalea" hakika "utaishia kutenda dhambi"
chukua hatua, tendea kazi hili somo,
dumu kwenye maombi na neno la mungu ili uwe na mamlaka itakayomfanya shetani akukimbie utakapompinga!
Mwl d.c.k
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675