Nchini Ujerumani imepitishwa sheria iliyoanza kutumika rasmi Ijumaa ya leo, Novemba Mosi, 2013 ambayo inawaruhusu wazazi kuchagua katika cheti cha kuzaliwa, kujaza jinsi ya tatu ambayo haitakuwa ya -ke wala -me kwa watoto wao.
Jinsi hiyo itatambulika kwa jina la 'haijaamuliwa' ikiwa inamaanisha kuwa mtoto aliyezaliwa ana mchanganyiko za jinsi zote mbili yaani za kike (-ke) na kiume (-me).
Sheria hiyo imelenga kuepuka kuwapa watoto wa aina ya jinsia ambayo si yao, na hivyo kuwaachia uhuru wa kuamua jinsia
waitakayo punde watakapokua na kujitambua na kuweza kufanya maamuzi kikamilifu kuhusu jinsi na jinsia yao.
Shirika la habari la Ujerumani linaripoti kwamba sheria hiyo ni matokeo ya ripoti ya mwaka jana kutoka kwenye Baraza la Maadili la Ujerumani ambalo liliishauri Serikali na Bunge kuhusu masuala tata ikiwa ni pamoja na kuachana na utaratibu unaowapa uhuru wazazi kuwachagulia watoto wao jinsi, kuamua kuhusu upasuaji na kuwapangia jinsia, watoto ambao wakikua na kujitambua hupatwa na hisia za kudhulumiwa. Limesema kwa mfano baadhi ya wanawake ambao walikatwa maumbile ya kiume kwa kuwa wazazi walitaka mtoto wa kike, baadaye walipojitambua walihisi kuwa walifanyiwa unyama na ukatili wa kukeketwa kiungo muhimu ambacho kama wangeachwa kukua na kujiamulia wenyewe, wasingekubaliana na upasuaji walizofanyiwa.
Mapendekezo mengine ya Baraza hilo pia yalisema shinikizo la kujaza katika rejista jinsi ya mtoto punde tu anapozaliwa, ni kuingilia haki binafsi za mtu ikiwa ni pamoja na haki ya kutaka kutibiwa ama la, kwa lengo tu la kutii matakwa ya Serikali.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani amesema wanatambua vyema kuwa sheria hiyo pekee haitakuwa suluhisho la mkanganyiko na utata wa jinsi lakini itasaidia kwa kiwango fulani.
Shirika la habari la Uingereza BBC linaripoti kuwa, takribani kiasi cha watu 2,000 wana tabia za mchanganyiko wa jinsi mbili na mara kadhaa watu waliofanyiwa upasuaji ili kubakiza jinsi moja, wamejikuta wakiishi kwa tabia za jinsia tofauti na jinsi zao na hivyo kulikuza badala ya kulitatua tatizo.
Ijapokuwa hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Ulaya kupitisha na kuanza kutumia sheria hii, zipo baadhi ya nchi ambazo zinaitumia sheria hii kama vile walivyofanya nchini Australia mwaka huu ambapo pia huwaruhusu watu kuwa na jinsia ya tatu katika pasi zao za kusafiria na kwenye vielelezo vingine vya Kiserikali.
Nchi nyingine ambazo ziliwapa raia wake haki ya kuamua jinsia zao kadiri walivyojitambua na kutaka kutambulika ni pamoja na India na Pakistani mwaka 2009 na Nepal mwaka 2007.