Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jumanne tarehe 22 October 2013, katika kanisa la Gilgal Christian Worship Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Waumini wakitafakari tukio hilo la uvamizi lililosababisha taharuki na sintofahamu kwa wakazi wa jiji la Mwanza. |
Wananchi wakitafakari tukio hilo nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza. |
tunaomba radhi kwa picha hizi |
Askofu wa kanisa hilo Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio hilo na akiiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.
Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi. |
Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza . |
sehem eneo likiwa na mabaki ya damu ambapo shambulio hilo lilifanywa na watu hao wasiojulikana |