PAPA Francis amemsimamisha kazi rasmi leo Askofu Franz-Peter Tebartz-Van Elst wa Limburg, baada ya kukumbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha kwaajili ya anasa na maisha ya kifahari.
Anatajwa kuwa hakuona aibu katika matumizi hayo makubwa kwani huwa wanapewa fedha kwaajili ya makazi ambayo huwa karibu na kanisa lakini yeye alichukua fedha zaidi na kuamua kuishi kwa anasa.
Na inaripotiwa kuwa anapotaka kutembea amekuwa akitumia magari ya kifahari tofauti na maaskofu wenzake walivyo au hata Papa Francis ambaye hivi karibuni alionesha mfano kwa kutumia gari kongwe aina ya Renault,(pichani chini) huku akionya juu ya maisha ya anasa kwa watu wanaopaswa kumtumikia Mungu.
Askofu huyo mwenyeji wa Magharibi ya Ujerumani ambaye amesababisha uongozi wa Kanisa Katoliki kukerwa na maisha ya anasa anayoishi kiasi kwamba ikawa gumzo kwa wananchi wa Ujerumani na Vatican kumjadili juu ya maisha ya anasa ya hali ya juu anayoishi.
Askofu huyu kabla ya kusimamishwa kazi amekuwa akiishi kama mwana mfalme na ametumia dola za kimarekani milioni 42 sawa na Sh za kitanzania bilioni 67.2 kwaajili ya ujenzi na ununuzi wa samani kadhaa katika kasri lake.
Vyombo vya habari vya ujerumani vimechapisha ushahidi wa picha na nyaraka zinazoonyesha katika kasri lake kuna sehemu ya kuogea iliyogharimu Euro 15,000(Sh milioni 33; meza ya mikutano ya Euro 25,000(Sh milioni 55) na kanisa dogo binafsi la Euro milioni 2.9 (Sh bilioni 6.6).
Siku mbili zilizopita
Mkuu wa maaskofu wa Ujerumani, Robert Zollitsch alimtaka Askofu Elst kujiuzulu wadhfa wake kutokana na kutumia fedha nyingi kwaajili ya kasri lake hilo katika kipindi ambacho Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis akiwahudumia masikini.
"Askofu wa Limburg anatakiwa ajiangalie mwenyewe na kubadilika...,"alisema Zollitsch.
Zollitsch ambaye ni miongoni mwa maaskofu wenye nafasi kubwa katika Kanisa Katoliki nchini ujerumani, aliahidi kulizungumza suala hilo la ufujaji wa fedha kwa Papa Francis ambaye alikwisha tangaza maaskofu waishi kwenye nyumba za kawaida na wasijifanye kama watoto wa kifalme.
Elst amekuwa akiishi kama mwana wa mfalme kwa kuiboresha kasri anayoishi ambayo ndani yake kuna vitu vya thamani kubwa.
(Hili ni mojawapo ya jengo la Askofu huyo |
Zollitsch hivi karibuni alisema anaiona hali ya Limburg kama "inahitaji uangalizi mkubwa na kufikiriwa sana."
Hivi karibuni alisema kuwa Kanisa la Ujerumani linatakiwa kupokea matokeo ya kashfa hiyo ambayo imeitingisha kwa sasa, kashfa ambayo ni sawa na kumpatia dozi nzito Papa Francis ambaye leo hii ameimaliza kazi.
Tayari vyombo vya habari vya ujerumani vimembatiza jina askofu huyo kama "Askofu wa anasa" mara baada ya ukaguzi wa mahesabu kubainisha ametumia fedha hizo kwaajili ya ujenzi na samani za kasri lake ikiwa ni mara sita ya gharama iliyopangwa.
Askofu Elst ambaye ujenzi wake umetumia mtindo wa ki-kale wa mradi wa Kikatoliki wa Papa mstaafu wa Ujerumani, Papa Benedict wa kumi na sita pia askofu huyo anatuhumiwa na mahakama nchini Ujerumani kwa kutoa kiapo cha uongo kuhusu kupanda ndege daraja la kwanza kutembelea miradi ya watu masikini nchini India.