Ukweli kuhusu Jaribu lako
Mara zote, ukiona Mungu ameruhusu jaribu linaloumiza moyo wako, hisia zako, imani yako nakadhalika kama ilivyokuwa kwa Ayubu, ujue "Mungu alikuwa anajisifu kuhusu wewe mbele ya shetani, na shetani akaomba ruhusa akuchokonoe, ili kumthibitishia Mungu kuwa hauko hivyo"na ili kulifanikisha hilo, anawinda imani yako ila kwa kupitia mazingira au matukio ambayo yatakufanya uamini ni mungu "anakutenda namna hiyo"
hata kwa Ayubu, shetani alitumia moto kuharibu mali za ayubu, lakini alihakikisha huo moto "utokee mbinguni" ili mwisho wa siku ayubu amlaumu, amhukumu au kumnung'unikia Mungu.
shetani anaweza kumtumia mchungaji wako, au mtumishi mwingine yeyote wa Mungu, au mkristo uliyemwamini na kumuona kioo, ili mwisho wa siku akuaminishe kuwa ni "Mungu anayekutendea hayo"
lengo lake anataka kuvuruga uhusiano wako na Mungu.
hata Yesu alijaribiwa na shetani kwa kutumia maandiko, ili ionekane kuna "kushiriki kwa Mungu" katika hilo.
hata siku moja usimlaumu Mungu, usimkasirikie Mungu, usimnung'unikie mungu kwa sababu ya jaribu lako!
bali mtukuze Mungu katikati ya majaribu; mwinue na kumbariki mungu katikati ya jaribu lako..." Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina lake libarikiwe"
lishinde jaribu kwa kumpa Mungu utukufu na kumwamini zaidi wakati wa jaribu badala ya kumkingia mgongo au kumkimbia.
Mwl Dickson Cornel Kabigumila.