Kukosekana kwa misingi bora ya kujisomea vitabu na makala mbalimbali kuanzia ngazi ya Familia hadi Vyuo vikuu imeelezwa kuwa ni moja ya chanzo cha umaskini wa kufikiri na ubunifu katika kazi miongoni mwa wasomi na wananchi wengi hapa nchini Tanzania,
Hayo yameelezwa na baadhi ya wachangiaji katika uzinduzi wa kitabu kipya chenye jina Wokovu ni Uhakika wa Maisha ya sasa na ya baadae, kitabu kilichoandikwa na Mwandishi James Kalekwa na kuzinduliwa jumapilii ya tarehe 10 March 2012 jijini Mwanza, na kuhudhuriwa na watu toka kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na wasomi wa vyuo vikuu vya jiji la Mwanza.
Miongoni mwa wachangiaji wahamasishaji waliochangia suala hili ni pamoja na MC Samuel Sasali na mchungaji Goodluck Kyara wa kanisa la New Vine Christian Center la jijini Mwanza
Kwa mujibu wa mchangiaji Samuel Sasali ameeleza kuwa tatizo kubwa la Elimu lililopo hapa nchini Tanzania ni matokeo mabovu ya misingi ya elimu tangu katika ngazi ya familia miongoni mwa watanzania waliowengi ambapo wengi wao hawana tabia ya kujishughulisha na usomaji wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitabu, hivyo kushindwa hata wao wenyewe kujiwekea mipangilio mizuri na vipaumbele vya maisha yao na watoto wao.
Mchungaji Goodluck Kyara katika kusisitiza suala la watu kujenga tabia ya kusoma vitabu ameeleza kuwa kila mafanikio huanza kama wazo ambalo huboreshwa kupitia kusoma vitu vitabu na makala mbalimbali hivyo kumsaidia mtu kupata maarifa zaidi na ubunifu wa kumuwezesha kufanya kitu kikubwa kitakachodumu kwa muda mrefu zaidi.
Aidha Mchungaji Kyara ,ameongeza kuwa shughuli yoyote ambayo hutumia nguvu zaidi kuliko akili matokeo ya shughuli hiyo hua ni ya muda mfupi tofauti na shughuli ambayo hutumia akili zaidi na nguvu kidogo ambapo mafanikio yake hua ni makubwa na ya muda mrefu na faida kwa watu wengi zaidi.
Mwandishi wa Kitabu hiki James Kalekwa ameeleza kuwa ,nia ya kuandika kitabu hiki ikiwa ni kuwafikia watu mbalimbali na kuwafikishia ujumbe kwamba Wokovu ni ni uhusiano baina ya Mwanadamu na Mungu,uhusiano mzuri utakaomfanya mwanadam kuishi maisha yenye amani katika misingi ya kiroho.
kuna watu wengi wanaishi maisha maovu na yasiyo na vipaumbele ,lakini dhamiri zao huwashtkai zikiwaonya kurudi kwenye wokovu ijapokuwa changamoto kubwa inayowakabili ni kukosa chombo cha kuwahamasisha katika kufanya mabadiliko hayo ya maisha yao , hivyo kupitia kazi za maandishi ikiwa ni pamoja na Kitabu hiki kipya kila atakayesoma kitabu hiki atapata hamasa mpya na nguvu katika kufanya mabadiliko ya maisha yake na kuweka vipaumbele vyenye tija katika maisha yake ya sasa na ya baadae.
Aidha Mwandishi wa kitabu hiki ameeleza kwamba Wokovu sio Dini au Dhehebu bali wokovu ni maisha halisi ya mwanadamu yanayompendeza Mungu kwa kuacha dhambi na kutenda mema hapa hapa Duniani.
Awali uzinduzi wa kitabu hiki ulitanguliwa na Ibada ya kusifu na kuabudu.matukio mengine yaliyojiri siku hiyo ni kama inavyoonekana katika picha.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wachangiaji katika uzinduzi wa kitabu kipya chenye jina Wokovu ni Uhakika wa Maisha ya sasa na ya baadae, kitabu kilichoandikwa na Mwandishi James Kalekwa na kuzinduliwa jumapilii ya tarehe 10 March 2012 jijini Mwanza, na kuhudhuriwa na watu toka kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na wasomi wa vyuo vikuu vya jiji la Mwanza.
Miongoni mwa wachangiaji wahamasishaji waliochangia suala hili ni pamoja na MC Samuel Sasali na mchungaji Goodluck Kyara wa kanisa la New Vine Christian Center la jijini Mwanza
MC Samuel Sasali moja ya wazungumzaji waliochangia michango yao ya mawazo katika uzinduzi huo |
Mchungaji Goodluck Kyara akisisitiza suala la watu kujenga tabia ya kusoma vitabu |
Aidha Mchungaji Kyara ,ameongeza kuwa shughuli yoyote ambayo hutumia nguvu zaidi kuliko akili matokeo ya shughuli hiyo hua ni ya muda mfupi tofauti na shughuli ambayo hutumia akili zaidi na nguvu kidogo ambapo mafanikio yake hua ni makubwa na ya muda mrefu na faida kwa watu wengi zaidi.
James Kalekwa Mwandishi wa Kitabu hiki akitoa ufafanuzi juu ya kitabu chake alichokiandika |
Mwandishi wa Kitabu hiki James Kalekwa ameeleza kuwa ,nia ya kuandika kitabu hiki ikiwa ni kuwafikia watu mbalimbali na kuwafikishia ujumbe kwamba Wokovu ni ni uhusiano baina ya Mwanadamu na Mungu,uhusiano mzuri utakaomfanya mwanadam kuishi maisha yenye amani katika misingi ya kiroho.
kuna watu wengi wanaishi maisha maovu na yasiyo na vipaumbele ,lakini dhamiri zao huwashtkai zikiwaonya kurudi kwenye wokovu ijapokuwa changamoto kubwa inayowakabili ni kukosa chombo cha kuwahamasisha katika kufanya mabadiliko hayo ya maisha yao , hivyo kupitia kazi za maandishi ikiwa ni pamoja na Kitabu hiki kipya kila atakayesoma kitabu hiki atapata hamasa mpya na nguvu katika kufanya mabadiliko ya maisha yake na kuweka vipaumbele vyenye tija katika maisha yake ya sasa na ya baadae.
Baraka Samson (Blogger ) akiifatilia mada zilizokua zikijadiliwa katika uzinduzi huo |
Mama mzazi wa Mwandishi James Kalekwa (wa kwanza kuli) |
Mzee Kalekwa (wa kwanza kulia) baba mzazi wa mwandishi James Kalekwa aliyeandika kitabu hiki |
Awali uzinduzi wa kitabu hiki ulitanguliwa na Ibada ya kusifu na kuabudu.matukio mengine yaliyojiri siku hiyo ni kama inavyoonekana katika picha.
Kikundi cha kusifu na kuabudu kikihudum kabla ya shughuli ya uzinduz wa kitabu hicho |
Kabula Siza |
Sephone Sospeter |
Pastor Innocent |
kutoka Kushoto ,Billy,na Denis Kiandika |
basi sawaaaaaaaaaaa moja ya kauli anazopenda kuzitumia MC Pilipili |
Mchungaji Goodluck Kyara na Samuel Sasali wakivunjwa mbavu na MC Pilipili |
MC Pilipili kazini |
Event Manager Adolf Nzwalla,(Kusho),Billy na Denis Kiandika |
MC Pilipili akifanya vitu vyake |
kutoka kushoto,MC Pilipili,Sowane Emanuel,Samuel Sasali,Baraka Samson |
Bloggers ,Samuel Sasali ,Sowane Emannuel,Baraka Samson |