Baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kutoka Geita wamekaa pamoja na kuondoa tofauti zao hususan katika suala la uchinjaji wa nyama kwa ajili ya kitoweo, miongoni mwa makubaliano waliyofikia ni nyama yoyote inayochinjwa kwa ajili ya biashara wachinje waislamu lakini kwenye sherehe zinazowahusu waislam wachinje waislamu na sherehe zinazowahusu wakristo wachinje wakristo wenyewe. Hivyo sherehe zozote za kidini wasiingiliane kwenye taratibu za kidini kwa kila mmoja.
Mhamasishaji katika mapatano hayo alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa magazeti ya Global publisher bwana Erick Shigongo pamoja na Mhariri wa gazeti la Championi,
katika mapatano hayo wakristo na waislamu walikumbatiana kuonesha wamemaliza tofauti zao na kisha kwa pamoja wakaungana na kwenda kwenye mechi ya fainali kati ya Buseresere na Katoro, ambapo Katoro walitwaa kombe.
Kabla ya kukabidhi kombe, masheikh na wachungaji walizungumza na kusisitiza sana suala la amani pia wakazungumzia mapatano yao baada ya kikao na mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakashangilia.
Mmoja wa viongozi wa serikali aliyehudhuria ni mbunge, Gaudencia Bukwimba CCM
Ikumbukwe hivi karibuni kulikuwa na machafuko huko Geita na kusababisha kifo cha mchungaji wa PAGT Mathayo Kachira. ambapo Waziri Stephen Wasira na Waziri mkuu Mizengo Pinda walijaribu kusuluhisha mgogoro huo bila ya mafanikio
Hali hii ilipelekea Mbunge wa Chadema Godbless Lema kutoa tamko lifuatalo
“Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara inayozidi imani , lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani“
source:http:strictlygospel.wordpress.com
Shehe Ismail Ibrahim na Mchungaji Isaya Ikiri |