Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA imetoa adhabu ya kuvifungia vituo vya Radio Kwa neema Fm ya jijini Mwanza,na Radio Imaan fm ya Morogoro kusitisha kurusha matangazo yake kwa muda usiopungua miezi sita,huku kituo cha radio Clouds FM cha jijini Dar es Salaam kikiamuliwa kulipa faini ya pesa taslim Tsh Milion 5 kuanzia sasa.
Kwa mujibu wa TCRA kituo cha Radio Kwa Neema FM ambacho ni kituo cha radio ya Dini ya kikristo kimehukumiwa adhabu hiyo kwa kile kilichoelezwa kua ni kukiuka maadili ya utangazaji kwa kufanya uchochezi hususani mikoa ya kanda ya ziwa katika suala la Uchinjaji wa nyama kwa kitoweo baina ya Wakristo na Waislam suala lililozua mgogoro mkubwa mkoa mpya wa Geita na Sengerema.
Kituo cha radio Imaan ambacho ni kituo cha radio kinachofuata misingi ya dini ya kiislam nacho kimefungiwa kwa kile kilichoelezwa kua ni kufanya kosa la kuhamasisha wananchi wa dini ya kiislam kususia zoezi la Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012
kituo cha Radio Clouds Fm cha jijini Dar es Salaam kimepewa adhabu ya kulipa faini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kwenda kinyume na maadili ya utangazaji kupitia kipindi chake cha Power Breakfast kinachorushwa live asubuhi chini ya watangazaji Gerlad Hando,Barbara Hassan na Paul James (PJ)
Katika kipindi hicho cha Powerbreakfast segment iliyosababisha kupewa adhabu hiyo ni segment inayojulikana kama Jicho La Ng'ombe ambapo kwa mujibu wa TCRA imeleeza kuwa kipindi hicho kinaenda kinyume na maadili.