Mtu mmoja anaesemekana kua ni mchungaji wa kanisa la PAG anadaiwa kupoteza Maisha katika vurugu kubwa zilizozuka mkoani Geita zilizohusisha mapigano makali baina ya Wakristo na Waislam katika eneo lijukanalo kama Buselele wilayani Chato Mkoa mpya wa Geita kutokana na mvutano kuhusu suala la Uchinjaji nyama kwa ajili ya kitoweo.
moja wa majeruhi katika vurugu hizo |
Chanzo cha mapigano hayo imedaiwa kuwa ni baada ya kuwepo kwa mgogoro wa mda mrefu kuhusu uchinjaji nyama baina ya wakristo na waislam mkoani Geita suala hilo lilichukua sura mpya baada ya wakristo kuanzisha mabucha yao kuuza nyama zinazodaiwa kuchinjwa na wakristo wenyewe kwa kile kilichodaiwa ni kutoshiriki kula nyama zilizochinjwa na watu wenye imani ya dini ya kiislam.
moja ya majeruhi katika vurugu hizo |
imeelezwa kuwa siku ya Jumatatu asubuhi ya tarehe 11 February 2013, mojawapo ya bucha eneo la Buselele wilayani Chato,mkoa wa Geita lilifunguliwa huku likiuza nyama zilizodaiwa kua zilikua zimetayarishwa na wakristo ndipo watu wanaosemekana kuwa ni wa imani ya dini ya kiislam walifika buchani hapo kutaka kuifunga bucha hiyo kitu kilichozua tafrani iliyopelekea askari wa kutuliza ghasia FFU kufika eneno hilo na kutaka kumchukua mwenye bucha hiyo.
mmoja wa majeruhi katika vurugu hizo |
katika mvutano huo mtu mmoja ambaye imeelezwa kua ni mchungaji wa kanisa la PAG amedaiwa kuuwawa kikatili kwa kupigwa mapanga katika vurugu hizo huku wengine wakijeruhiwa vibaya.
Bi Helen Kijo Bisimba mmoja wa wanaharakati wa Haki za Binadamu ameelezea tukio hilohuku akitoa wito kwa serikali kulishughulikia tatizo hili kwa kulichukulia hatua madhubuti zitakazoleta suluhisho la kudumu
"Masuala kama haya yatazamwe kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia haki za binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa ibada na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.
Lakini pia njia za utatuzi wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi yamaongezi ya kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro"