Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Stara Thomas ambaye awali alitangaza kuokoka na kuanza kurekodi nyimbo za
Injili,ametangaza kurudi tena katika muziki wa bongo flava.
Stara Thomas aliyewahi kutangaza kwenye vyombo vya habari uamuzi wake wa kuokoka na kuachana na muziki wa bongo flava na kuhamia kwenye muziki wa injili wiki hii ameshtua wengi baada ya kusema kuwa ameamua kurudi tena kwenye muziki wa bongo flava.
katika kunukuuu moja ya habari iliyotolewa mwaka 2011 kupitia vyombo vya habari Stara Thomas alisema
“Nilipata wito kutoka kwa Yesu kwa kuwa aliwaita watu wote wasumbukao na kulemewa na mizigo waende kwake atawapumzisha”
source:Jamii Forum
baada ya kutangaza uamuzi huo wa kuokoka stara Thomas alikua akiabudu kwenye kanisa la Shalom lililoko Mbezi Salasala!
Akiongea kupitia kituo cha Clouds TV na pia habari hiyo kurushwa na Clouds FM radio kwenye kipindi cha Amplifaya cha jumanne 8 January 2013 habari ilikua ni kwamba Stara Thomas anatarajia kutoa nyimbo mpya akishirikiana na mwanamuziki Linex
Mwanamuziki Linex |
Mwanamuziki Linex alisema kwamba ameamua kufanya wimbo na Stara Thomas kwa sababu kwanza anamkubali sana StaraThomas kama Mwanamuziki mwenye uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi popote tofauti na wasanii wengine wa bongo flava ambao wao ni wasanii wa studio tuu lakini inapokuja suala la kuimba hata kwenye live band wanakua hawana uwezo huo.
Mnamo Mwaka 2012 mwezi June pia katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya stara Thomas na Mtangazaji Millard Ayo wa Clouds Fm Stara aliwahi kueleza kusikitishwa kwake na wanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania kwa namna ambavyo stara alidai kua ni wabinafsi....
Hiki ndicho alichokisema stara wakati huo,,,
“kuna ubinafsi kuna roho nyingine zinazotembea sio kama kwenye bongofleva tulikua tunaupendo, ukinikosea mimi nakwambia tumemaliza yani hata majungu yalikua sio kiivyo lakini huku ni live, yani unamuona mtu moja kwa moja moyo wake hautaki” source:http://millardayo.com/sababu-za-stara-thomas-kusema-kwenye-muziki-wa-injili-kuna-unafiki-mkubwa/
"mwanzoni wakati nataka kuwashirikisha wasanii wakubwa wengine imekua ngumu kwa sababu nimegundua kuna unafiki mkubwa sana, mtu anaweza kukuchekea machoni lakini moyoni ni muongo, kuna wasanii wengine wakubwa niliwaona lakini nilipowakaribia nikagundua sio”
source:http://millardayo.com/sababu-za-stara-thomas-kusema-kwenye-muziki-wa-injili-kuna-unafiki-mkubwa/
Wanamuziki wengine toka Afrika Mashariki ambao nao pia walishawahi kutangaza kuanza kuimba nyimbo za injili na baadae kurudi kwenye Miziki ya Dunia ni pamoja na Kidum Na DNA kutoka Kenya.
Mwanamuziki DNA |
Mwanamuziki Kidum |
Hebu post nyimbo moja ya injili aliyofanya stara...aache maneno tu ...yeye alikua anafuta soko
ReplyDeleteJueni kuwa HAO WANAO-ONGOZWA NA ROHO HAO NDIO WANA WA MUNGU.na MTU ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO ..HUYO SIO WAKE9uSIPOKUWA NA Roho Mt wewe si mtu wa Kristo YESU.
ReplyDeletesi rahisi hekalu la Mungu kushirikiana na hekalu la beliari.
Warumi.8:9-14