Naibu spika wa bunge la Israel Danny Danon ambaye pia ni mshirika mkubwa wa chama tawala nchini Humo ,Likud, kinachoongozwa naWaziri mkuu wa Israel bwana Benjamini Netanyahu amesema kwamba Taifa la Israel halitayumbishwa wala kutegemea sera za Rais Barack Obama wa marekani katika utendaji wa nchi hiyo.
|
Danny Danon Naibu spika wa bunge la Israe |
Katika moja ya maelezo yake aliyoyatoa kuhusu ushindi alioupata Rais Obama kuliongoza taifa la Marekani kwa kipindi cha miaka mingine minne,Danon amesema kwamba ushindi wa Obama ni wazi unatoa taswira kwamba taifa la Israel lazima lijisimamie lenyewe hususan katika maslahi yake katika sera za kimataifa.
|
Danny Danon Naibu spika wa bunge la Israe |
|
“Hatuwezi kumtegemea mtu yoyote isipokuwa sisi wenyewe, kwa sababu tumeona namna gani Obama ameiathiri Marekani kutokana na uongozi wake kujawa na sera mbovu hususan katika sera za kimataifa ambazo dhahiri zimekuwa zikipendelea nchi za kiarabu duniani dhidi ya nchi za magharibi na dhidi ya Israel.”
@Danny Danon
Wakati huohuo Hivi karibuni msuluhishi mmojawapo toka mamlaka ya kipalestina akionesha kupata matumaini kutokana na uongozi wa Rais Obama yeye alidai kwamba endapo Obama akifanikiwa kushinda na kupata nafasi ya kuongoza Marekani kwa miaka mingine minne,ni dhahiri ataitumia fursa hiyo dhidi ya Benjamin Netanyahu Waziri mkuu wa Israel ambaye anachukuliwa kama kikwazo kikubwa katika mazungumzo ya kuleta amani mashariki ya kati.
|
Benjamin Netanyahu ,Waziri mkuu wa Israel |
Msuluhishi huyo anaenda mbali zaidi kwa kusema kwamba Obama aliahidi pia katika kampeni za kipalestina kwenye Umoja wa mataifa, kuboresha Baraza la usalama la umoja wa mataifa, katika maadhimio namba 242, ambayo yanaamuru serikali ya kipalestina kustawishwa katika ,miji ya West Bank ,ukanda wa Gaza na Jerusalem mashariki
|
Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel
|
Msuluhishi huyo anasema kwamba ikulu ya Marekani iliwataka wapalestina kuacha mapigano kwani moja ya ajenda kuu ambazo Obama atazishughulikia pindi atakapo ingia madarakani kwa miaka mingine minne itakuwa ni kuhakikisha serikali ya kipalestina inastawishwa
|
Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel |