Baada ya vurugu zilizotokea siku ya Ijumaa yaliyohusisha uchomaji moto makanisa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh.Jakaya Mrisho Kikwete afanya ziara kwenye makanisa hayo kujionea mwenyewe uharibifu uliofanywa.
wakati huo huo Rais Kikwete amelitaka Jeshi la polisi kuwachukuliwa hatua wote waliohusika na vitendo hivyo vyote huku akiitaka jamii kuishi kwa upendo na kuheshimiana ikiwa ni pamoja na kuheshimu dini ya kila mmoja ili kulilinda taifa kutotumbukia katika machafuko ya Kidini
picha kwa hisani ya Kishindo leo blog
Rais Kikwete akionyeshwa mimbari iliyoharibiwa katika vurugu hizo |
Rais Kikwete akionyeshwa Gari la Mchungaji Joseph Kinyota wa TAG Mtoni Kijichi lililochomwa moto katika kanisa hilo |