Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Upendo Nkone anatarajiwa kuperfom nchini Marekani katika tamasha kubwa la muziki wa injili litakalofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 1 na 2jumapili, September 2012 katika mji wa Ohio, Columbus nchini Marekani.
Wanamuziki wengine watakaopanda steji mmoja na Upendo Nkone nchini Marekani ni pamoja na Felis Mubibya toka nchini Congo DRC,Michele Hakizimana toka Burundi,Prexy Sam Ola toka Nigeria,huku timu ya wachungaji ikiwa ni pamoja na pastor Daniel Mutambo toka Congo DRC,na pastor Gerri Brown toka USA nao wakiwa pamoja katika tamasha hili kubwa sana.
Waandaaji wa Tamasha hilo pastor Donnis na NnunuNkone wa All Nations breakthrough church ameeleza kuwa katika tamasha hilo watu watakao hudhuria watapata fursa ya kusifu na kuabudu kwa muziki saafi toka kwa wanamuziki toka africa pamoja na chakula cha pamoja kwa wote watakoahudhuria huku kesho yake siku ya jumatatu yake itakuwa ni labor day ambapo ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi .
Mwanamuziki wa Nyimbo za injili nchini Tanzania Upendo Nkone |
Upendo Nkone (katikati),Upendo Kilahiro kulia walipotembelea Voice of America nchini Marekani |
Mwanamuziki Felis Mubibya toka Congo DRC |
Prexy Sam Ola toka Nigeria |
Mwanamuziki Prexy Sam Ola toka Nigeria |
Pastor Donnis &Nnunu Nkone wa All Nations Breakthrough church nchini Marekani ni waandaaji wa tamasha hilo |
Pastor Donnis Nkonne wa All Nations Breakthrough church nchini Marekani |