Tarehe 11 na 12 siku ya Jumamosi na Jumapili ya wiki hii wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watapata fursa ya kushuhudia tamasha kubwa sana lililopewa jina la IPENDE TANZANIA na Andrew Palau litakalofanyika katika viwanja vya Jangwani,huku wanamuziki toka Marekani ,Don Moen,Nicole C.Mullen, na Dave Lubben wakitarajiwa kupiga Live Nyimbo zao mbalimbali zilizowahi kutamba katika ulimwengu wa Gospel Music Duniani.
Mwinjilist Andrew Palau |
Andrew Palau mhimili mkubwa katika tamasha hili ambalo litafanyika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza historia yake inaoyesha kuwa yeye ni mmoja kati ya watu ambao ni matokeo ya Mabadiliko yaliyotokana na Nguvu ya Mungu iliyomtoa kutoka katika njia mbaya ya maisha yasiyompendeza Mungu aliyokuwa akiishi hapo awali.
Maisha yake yalibadiliaka kwa kiasi kikubwa sana na kuanza kufanya huduma ya kumtumikia Mungu baada ya kuishi miaka 27 mbali na Yesu
Andrew Palau na mkewe ajulikanaye kwa jina la Levy Wendy wamebarikiwa kuwa na watoto watatu, ambao ni Christopher, Jonathan na Sadie Anne. wote kwa pamoja wanaishi Portland, Oregon karibu na Makao makuu ya Huduma ya Palau.
Watoto wa Andrew Palau |
Baada ya kuhitimu shahada ya Fasihi ya Kiingereza, Andrew alikwenda Boston ambako alifanya kazi kwa miaka mitano na baadae Mnamo mwaka wa 1993, Andrew alichukua likizo ili kujiunga na wazazi wake kwa ajili ya uinjilisti na Shirika la kiinjilisti la Luis huko Kingston, Jamaica.
Baba yake alihubiri ujumbe ule ule wa Injili ambao alishamsikia akiuhubiri mara nyingi, lakini mara hii ulikuwa tofauti. kupitia Baba yake Andrew Palau alishuhudia uwepo wa Mungu katika maisha ya baadhi ya wajamaica aliokutana nao, ikiwa ni pamoja na Levy Wendy ambaye baadaye alifunga naye ndoa.
Mwinjilist Luis Palau akihudumu kwa Makumi elfu ya watu katika Jiji la ho Chi Minh nchini Vietnam katika tamasha la kuadhimisha miaka 100 ya kanisa la kiprotestant |
Andrew alikuwa mtu muhimu katika kuandika maudhui ya Tamasha za kwanza za Palau ambapo mlikuwa na mabadiliko muhimu yaliyoonyesha tofauti na mtindo wa uinjilisti wa mikutano ya nje.
Tamasha mbili za kwanza zilifanyika katika wigo wa nyumba ya Palau huko Portland, Oregon, mwaka 1999 na 2000. Hii ilkuwa kabla ya kutembelea maeneo mengine ya nchi na kuwa na tukio moja katika ukumbi wa kitaifa huko Washington DC
Andrew Palau amekuwa akifanya matamasha katika nchi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Romania, Misri, Mexico, India, Poland, na Jamaica. Yeye amehubiri Injili kwa mamilioni ya watu, na katika kila fursa yeye huonyesha mvutio wa hisia na upendo kwa Kristo na uinjilisti sawa sawa na ule alionao baba yake.
Mwaka 2009, alijiunga na Luis katika makala yake ya redio ya Kufikia Dunia Yako na Luis Palau. Ujumbe wa dakika mbili wa Andrew hutangazwa kwenye stesheni za redio 855 kila Ijumaa.
“Kuna nguvu iletayo mabadiliko katika Yesu Kristo, msalaba, damu yake, kuzikwa kwake, na kufufuka kwake,” anasema Andrew. “Ninatamani kuona watu wote wakipata zawadi yake ya msamaha wa dhambi, Roho Mtakatifu awatie nguvu, na uhakika wa mbinguni milele.”