Dk. Steven Ulimboka amerejea jumapili hii 12 August 2012 nchini na kutoa shukrani za dhati kwa
watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi
kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa
madaktari.
Ulimboka
amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani
hasa aliyemteka na kumpa mateso makali Dk. Steven Ulimboka ambaye ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu ya wananchi sasa ni
kutaka kujua ukweli kupitia kwake.
Daktari
huyo ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na
maslahi ya madkatari na huduma bora Hospitalini amerejea jijini Dar
es Salaam akitokea nchini Afrika kusini ambako alipelekwa na Madaktari
wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa akitibiwa majeraha
aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.
Dk.
Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya
Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari huyo ni raia wa Kenya
ambaye tayari wanamshikilia.
Dk. Ulimboka amewasili majira ya saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na SA Airways na kulakiwa kwa
shangwe, hoihoi nderemo na vifijo kutoka kwa ndfugu jamaa na marafiki
sambamba na madaktari wenzake na wanaharakati.
“Nimepona
ndugu zangu….nawashukuru nyote mlioniombea, watanzania, madaktari,
ndugu na jamaa zangu nashukuru pia kunisaidia kupata matibabu bora hadi
leo hii narudi nyumbani, niko fiti nikitembea mwenyewe,” alisema Dk. Ulimboka.shukurani kwa blogger father Kidevu "FK"