Kundi la Music wa Gospel la New life band limendesha kambi la vijana mkoani Kigoma ambapo zaidi ya vijana 700 kutoka mikoa ya magharibi mwa Tanzania wamekusanyika pamoja mkoani hapo katika kambi hilo la wiki moja lililofanyika Bigabiro mission na kupata mafundisho mbali mbali hususan katika masuala ya, ki Biblia,Kijamii na kiuchumi yenye Lengo la kuwajenga vijana kiroho na na kimwili pia.
moja ya masomo yalikuwa yakifundishwa katika kambi hilo ni mahusiano ambapo somo hilo lilifundishwa na Mwl.sostenes Mabele.
moja ya masomo yalikuwa yakifundishwa katika kambi hilo ni mahusiano ambapo somo hilo lilifundishwa na Mwl.sostenes Mabele.
pamoja na mafundisho hayo pia kundi hilo limefanya matamasha ya kusifu na kuabudu katika mkoa huo wa kigoma ambayo yamehudhuriwa na mamia ya watu na kumsifu Mungu kupitia huduma ya kusifu na Kuabudu .