Mwanamuziki wa kimataifa wa nyimbo za injili Don Moen pamoja na Nicole Mullen ambaye alitamba sana na songi my redeemer lives kwa pamoja wanatarajiwa kulitikisa Jiji la Dar es salaam siku ya tarehe 11 na 12 ya mwezi Agosti mwaka huu 2012 katika Tamasha kubwa lililopewa jina la IPENDE TANZANIA au LOVE TANZANIA na Andrew PALAU litakalofanyika katika viwanja vya Jangwani kuanzia majira ya saa saba mchana hadi saa mbili usiku.
Mwanamuziki mwingine atakayeambatana na Don Moen na Nicole Mullen ni Dave Lubben
Wanamuziki hao kwa pamoja wanatarajiwa kuushusha uwepo wa Bwana katika viwanja vya Jangwani,Dar es salaam na kuwapa fursa wakazi wa Jiji la Dar na wote watakaotoka mikoani na kwenda Dar kuhudhuria tamasha hili kubwa na la aina yake kupokea Nguvu za Mungu katika kusifu na kuabudu.
kutoka Tanzania hadi sasa wanamuziki watakaopanda katika stage moja na Don Moen ni pamoja na Christina Shusho,kundi la The Voice,John Lisu, Masanja Mkandamizaji, na kikundi cha Praise and worship
wakati hayo yote yakitarajiwa kufanyika, kwa upande mwingine maandalizi kwa upande wa vikundi vya PRAISE AND WORSHIP yameendelea katika kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church "DPC " ambapo mazoez ya praise yameanza kwa ajili ya tamasha hilo
Tazama hii Video ili kuona namna mazoez ya praise and worship yanavyoendelea special kwa tamasha hili la Ipende Tanzania
zaidi sana kuhusu Tamasha hili Tazama hii Video hapa chini
Nicole Mullen hapa akiimba My Redeemer Lives, nyimbo hii na nyingine nyingi zitapigwa live kwenye Tamasha hilo 11-12 Agosti |
Nicole Mullen |
Nicole Mullen |
Mwanamuziki Dave Lubben |
kutoka Tanzania hadi sasa wanamuziki watakaopanda katika stage moja na Don Moen ni pamoja na Christina Shusho,kundi la The Voice,John Lisu, Masanja Mkandamizaji, na kikundi cha Praise and worship
Christina Shusho mmoja wa wanamuziki toka Tanzania atakayepanda stage moja na Don Moen siku hiyo |
Christina Shusho mwanamuziki toka Tanzania nae ataonyesha umahiri wake katika kumwimbia Mungu katika Tamasha hilo |
Kundi Maarufu kwa Acapella nchini Tanzania, almaarufu kama THE VOICE nao wamejipanga kisawasawa kuonyesha uwezo wao wa kupiga Acapella mbele ya Don Moen na Nicole Mullen siku hiyo |
Tazama hii Video ili kuona namna mazoez ya praise and worship yanavyoendelea special kwa tamasha hili la Ipende Tanzania
zaidi sana kuhusu Tamasha hili Tazama hii Video hapa chini