tarehe ya kusikilizwa kwa kesi inayomkabili mchungajiYoucef Nadarkhani imeripotiwa kutangazwa kuwa september 8
Mchungaji Youcef Nadarkhani mwenye umri wa miaka 35 kutoka Rasht,Iran amegusa mioyo ya wakristo wengi duniani kote kwa msimamo wake thabiti katika imani yake ya kikristo licha ya kukabiliwa na adhabu ya kifo kutokana na kosa la kuwa mkristo nchini Iran moja ya nchi za kiislam na zinazoongozwa kwa sheria za kiislam.
kwa mujibu wa huduma ijulikanayo kama Present Truth Ministries, ambayo imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu sana kesi ya mchungaji Nadarkhani imeleezea kuwa mchungaji Nadarkhani anatarajiwa kukabiliwa na kesi ya jinai ya kiusalama
katika barua yake ya hivi karibuni aliyoiandika mchungaji Nadarkhani ambayo ilitolewa mwez may mwaka huu 2012 kwa wote walioguswa na kesi yake Nadarkhani alisema,
" Nahitaji kuwakumbusha wapendwa wangu kwamba japo kesi yangu imechukua mda mrefu ,kimwili natamani siku ziishe, lakini nimejikabidhi kwa Mungu na mapenzi ya Mungu yatimie"
Nadarkhani, mchungaji kutoka katika huduma ijulikanayo kama network of house churches, alikamatwa Oct. 13, 2009, baada ya kupinga uamuzi wa serikali ya Iran kuwalazimisha watoto wote nchini Iran akiwemo na mtoto wake kusoma Quran.
mwanzoni Mchungaji Nadarkhani alishitakiwa kwa makosa ya kuweka pingamizi kwa serikali ya Iran lakini baadae kesi ilibadilika na kuanza kushitakiwa kwa makosa ya kufanya huduma ya kitume na uinjilist kwa Waislam .
mwaka 2010,Nadarkhani alihukumiwa adhabu ya kifo na hukumu hiyo ilitolewa na mahakama kuu ya Iran Mwaka jana.
mwaka 2010,Nadarkhani alihukumiwa adhabu ya kifo na hukumu hiyo ilitolewa na mahakama kuu ya Iran Mwaka jana.
kwa mujibu wa sheria ya kiislam ijulikanayo kama "Islamic Sharia Law", mchungaji au mtume kama Nadarkhani anapewa siku tatu ili kuikana imani yake ya kikristo na kuingia katika imani ya kiislam lakini licha ya kupewa hiyo nafasi ,mchungaji Nadarkhani alikataa kuikana imani yake ya kikristo.
hivi sasa huduma ya Truth Ministries na mashirika mengine yamekuwa yakipinga hadharani adhabu hiyo na kuomba maombi na msaada mbalimbali kwa viongozi wa nchi na serikali zao ili kumuokoa mchungaji Nadarkhani kutoka katika adhabu hiyo ya kifo inayomkabili
Bunge la Marekani limetoa maazimio hivi karibuni zikishutumu kuwekwa na kuhukumiwa kwa mchungaji Nadarkhani na kuitaka serikali ya Iran kumwachilia Haraka mchungaji Nadarkhani