Sakata la kutekwa kwa kiongozi wa Jumuiya ya madaktari, Dkt. Steven Ulimboka limechukua sura mpya, baada ya kuibuka taarifa nyingine zinazodai kuwa, mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za utekaji na utesaji wa kiongozi huyo anamatatizo ya akili.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,JosephatGwajima,ameeleza kushangazwa
na taarifa ya Jeshi la Polisi kwamba mtuhumiwa
aliyehusika kumteka kiongozi huyo, alikwenda kutubu katika kanisa lake.
Mbali na kushangazwa na taarifa hiyo, Askofu Gwajima pia alilitaka jeshi hilo kutolihusisha kanisa lake na mtuhumiwa huyo, Joshua Mhindi ambaye ni raia wa Kenya.
Askofu huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, kutokana na taarifa ya polisi kujikanganya anahisi kwamba mtuhumiwa huyo ametumwa ili kulivuruga kanisa lake.
Askofu Gwajima alitoa msimamo huo jana, katika Ibada iliyofanyika viwanja vya Tanganyika Parkers, eneo la Kawe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni huduma maalumu ya maombezi kwa waumini wake.
Akisimulia tukio la mtuhumiwa huyo kufika kanisani kwake, Askofu Gwajima alisema, Juni 26 mwaka huu, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa walinzi wa kanisa hilo kuwa ni raia wa Kenya, aliomba kuonana na kiongozi wa kanisa hilo, ili amweleze jambo zito alilonalo moyoni.
Alisema walinzi walipomhoji zaidi kuhusu jambo hilo, alidai kuwa yeye ni mmoja kati ya kundi lililohusika kumteka kwa lengo la kumuua Dkt. Steven Ulimboka, hivyo alitaka kutubu kwa kiongozi huyo wa kanisa.
Askofu Gwajima alisema, kutokana na maelezo yake walinzi wake wakiongozwa na mtu aliyemtaja kwa jina moja la Joseph Marwa, waliamua kumpeleka katika Kituo cha Polisi Kawe ambako walimkabidhi kwa polisi na kuandikisha maelezo yake.
“Katika mahojiano hayo, mtu huyo alitaja nyumba ya kulala wageni alikokuwa amepanga (guest house) iitwayo My Fair, ambayo iko jirani kabisa na kituo cha Polisi Kawe. Inakuwaje Kamanda Kova anasema mtu huyu alipanga hoteli kati kati ya mji?
“Baada ya siku chache, polisi wa makao makuu walikuja hapa kanisani wakiongozana na mtuhumiwa wakidai kwamba wameelezwa na mtu huyo kwamba anatabia ya kuropoka ovyo, na anasumbuliwa na matatizo ya kichwa, hivyo maelezo aliyoeleza awali kanisani hayakuwa sahihi.
“Polisi walisema mtu huyo ameomba msamaha kwa sababu huwa ana matatizo ya kuropokaropoka, hivyo tumsamehe.
“Polisi walioandamana na mtuhumiwa kutoka makao makuu ya polisi wakasema, kwa sababu alikuja mwenyewe na amekiri kuwa maelezo yake ya awali aliyoyatoa kwetu alikuwa ameropoka tu hivyo anaomba msamaha, polisi wakashauri suala hilo liishie hapo, wote tukiamini kwamba mtu huyo ana matatizo ya akili.
“Kilichokuja kutushangaza baadaye ni kumsikia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova Juni 13 mwaka huu, kuibuka na kusema mtuhumiwa huyo kakamatwa baada ya yeye kujisalimisha kanisani kwetu.
“Kwanza Kanisa langu halina utaratibu wa kutubu, na kama ungekuwepo kamwe tusingetangaza, kwani toba ya mtu huwa haitangazwi, kwa sababu hiyo natangaza kwamba kanisa lisihusishwe na mtuhumiwa huyu” alisema Askofu Gwajima na kushangiliwa na waumini.
“Naomba polisi wasihusishe kanisa letu na mtu huyu, watu wananipigia simu na kuniuliza, Mkenya huyu amepajuaje Mabwepande? na mimi sijui……
Wakati taarifa ya Askofu inasema, mtuhumiwa alipanga nyumba ya kulala wageni ya May Fair, na tayari polisi walishamuona kuwa hana akili timamu, ameshangazwa na kufunguliwa mashitaka mtu ambaye awali alionekana hana akili timamu.
Hata hivyo Askofu Gwajima aliitaka Serikali iunde tume huru ya uchunguzi wa suala la kutekwa kwa Dkt. Ulimboka na kamwe kazi hiyo isiachwe ifanywe na polisi peke yao.
na taarifa ya Jeshi la Polisi kwamba mtuhumiwa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,JosephatGwajima |
Mbali na kushangazwa na taarifa hiyo, Askofu Gwajima pia alilitaka jeshi hilo kutolihusisha kanisa lake na mtuhumiwa huyo, Joshua Mhindi ambaye ni raia wa Kenya.
Askofu huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, kutokana na taarifa ya polisi kujikanganya anahisi kwamba mtuhumiwa huyo ametumwa ili kulivuruga kanisa lake.
Mkusanyiko wa waumini katika kanisa la Askofu Gwajima lililopo viwanja vya Tanganyika Parkers, eneo la Kawe jijini Dar es Salaam |
Akisimulia tukio la mtuhumiwa huyo kufika kanisani kwake, Askofu Gwajima alisema, Juni 26 mwaka huu, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa walinzi wa kanisa hilo kuwa ni raia wa Kenya, aliomba kuonana na kiongozi wa kanisa hilo, ili amweleze jambo zito alilonalo moyoni.
Alisema walinzi walipomhoji zaidi kuhusu jambo hilo, alidai kuwa yeye ni mmoja kati ya kundi lililohusika kumteka kwa lengo la kumuua Dkt. Steven Ulimboka, hivyo alitaka kutubu kwa kiongozi huyo wa kanisa.
Askofu Gwajima alisema, kutokana na maelezo yake walinzi wake wakiongozwa na mtu aliyemtaja kwa jina moja la Joseph Marwa, waliamua kumpeleka katika Kituo cha Polisi Kawe ambako walimkabidhi kwa polisi na kuandikisha maelezo yake.
“Katika mahojiano hayo, mtu huyo alitaja nyumba ya kulala wageni alikokuwa amepanga (guest house) iitwayo My Fair, ambayo iko jirani kabisa na kituo cha Polisi Kawe. Inakuwaje Kamanda Kova anasema mtu huyu alipanga hoteli kati kati ya mji?
“Baada ya siku chache, polisi wa makao makuu walikuja hapa kanisani wakiongozana na mtuhumiwa wakidai kwamba wameelezwa na mtu huyo kwamba anatabia ya kuropoka ovyo, na anasumbuliwa na matatizo ya kichwa, hivyo maelezo aliyoeleza awali kanisani hayakuwa sahihi.
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Bw.Suleiman Kova |