Kanisa la E.A.G.T Lumala mpya chini ya Uongozi wa Mch.Dr.Daniel Moses Kulola lililopo Jijini Mwanza limeandaa tamasha la kusifu na Kuabudu linalotarajiwa kufanyika jumapili hii ya tarehe 01July 2012 katika uwanja wa wazi wa kanisa hilo ikiwa ni ishara ya kurudisha sifa na shukurani kwa Mungu kwa mema yote aliyotenda kwa watu wake katika kipindi cha mwezi mzima.
akiongea na Blog hii Mchungaji wa kanisa hilo Mch.Dr Daniel Moses Kulola amesema kuwa lengo la tamasha hili ni kumpa Mungu sifa na utukufu kama shukurani kwa yale yote ambayo Mungu ametenda maishani mwetu.
"""Mungu anapenda sifa, watu wengi wamekuwa wanafanya matamasha ya kutolesha pesa na yanageuka si kumtukuza Mungu it is a business, ila sisi tuna fanya bure na Pia mwisho tunatoa zawadi kwa kila choir itakayo kuja, just to Encourage their ministry, ni kitu cha kipekee sana..... na tunafanyia nje eneo la wazi.."""
katika tamasha hilo litakalofanyika jumapili hii ya tarehe 01july2012 vikundi mbali mbali vya uimbaji vinatarajiwa kupanda kwenye jukwaa siku hiyo na kumtukuza Mungu kwa uimbaji.
miongoni mwa vikundi vinavyotarajiwa kuwepo na kuimba siku hiyo ni pamoja na Kihayile Group,Akrama Band,Mwanza Singers,Mwanza Gospel,Uinjilist Choir,Ufunuo Choir, Bugando Divine singers, Msumbiji wana dawa ya ndoa, Mlima wa utukufu ya ilemela kwa mch Gecha, Jordan choir, Eagt igombe, Uinjilisti Gilgali, AIC pasiansi, EAGT imani Pasiansi, Calvary Assemblies choir, EAGT Ibungilo.
wenyeji wa Tamasha hili ni Uinjilisti kwaya, Ufunuo kwaya na Upendo choir na Akrama Band,ambazo zote ni kwaya na band zilizopo katika kanisa hilo la EAGT Lumala mpya.
Tamasha hili la kusifu na kuabudu linakuja ikiwa ni moja ya utaratibu ambao kanisa hilo limejiwekea kila inapotimia mwisho wa mwezi kwaya na vikundi mbali mbali vya uimbaji vya jijini mwanza hukutana pamoja kanisani hapo na kufanya Tamasha lisilo na kiingilio katika viwanja vya kanisa hilo na Kumsifu Mungu kupitia Music na uimbaji,na pia kuinua vipaji na huduma za waimbaji ili waweze kusonga mbele katika huduma ya kusifu na kuabudu.
kanisa hilo linapatikana mtaa wa Lumala Mpya karibu na soko la SABASABA ,na pia ni karibu na njia ya kuelekea Mtaa wa Kiseke.Jijini Mwanza.