Mwanamuzi wa Injili toka Afrika Kusini anayefahamika kama S' fiso Ncwane amefariki dunia siku ya jumatatu saa 3asubuhi akiwa hospitali nchini Afrika Kusini kutoka na kile kinachodaiwa kua ni tatizo la Figo.
Taarifa hiyo imethibitishwa na dada yake anaitwae Gugu. na pia msemaji wa familia Sipho Makhabane amethibitisha taarifa hiyo na kusema mwanamuziki huyo alifariki majira ya saa saa 3asubuhi leo
Taarifa hiyo imethibitishwa na dada yake anaitwae Gugu. na pia msemaji wa familia Sipho Makhabane amethibitisha taarifa hiyo na kusema mwanamuziki huyo alifariki majira ya saa saa 3asubuhi leo
" Nathibitisha ni kweli amefariki asubuhi ya leo hospitali na bado uchunguzi unaendelea japo inaonekana figo zilifeli"
Mwanamuziki huyu aliweza kung'aa kwenye vichwa vya habari mwaka jana baada ya kumnunulia mchungaji wake gari aina ya Mercedes yenye thamani ya Randi 1.9milion na kusema Mchungaji huyo aliweza kuokoa maisha yake kupitia maombi aliyokua akimuombea na hivyo hana budi kurudisha fadhila.
Ncwane alikua ndiye mwanamuziki wa kwanza wa nyimbo za injili kushinda Rekodi ya mwaka 2013 katika tuzo za South African Music Awards akiwa na hitsong yake "Kulungile Baba"
Mwanamuziki huyu ameacha mke na aitwaye Ayanda Ncwane na watoto wawili
Mwanamuzi huyo anafahamika kwa wimbo alioufanyia Remix wa "When Jesus Say"
Baadhi ya video zake zingine ni pamoja na hii hapa