Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Lightness Kivuyo, mkazi wa Unga Limited jijini Arusha, amefariki akiwa anaombewa nyumbani kwa mchungaji anayejulikana kama 'Nabii Rajabu' eneo la kwa - Mrombo
Dada wa marehemu, Juliana Kivuyo amesema kuwa ndugu yake alikuwa anaumwa na alipelekwa na mumewe kwa ajili ya maombezi kwa Nabii Rajabu lakini alianguka miguuni wa mtume huyo na kufariki dunia wakati huduma ya maombezi ikiendelea
"Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi "alisema
Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia huduma hiyo
Anasema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio alimkuta ndugu yake akiwa amelazwa kwenye kochi akiwa bila nguo na akiwa hana nyusi ambapo mwili wake ulikuwa umefunikwa na khanga na tayari alikuwa ameshafariki.
Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa katika Hospital ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo, walipokea mwili wa Lightness huku waliomleta wakidai kuwa wamemleta mgonjwa na sio marehemu, lakini baada ya kumpima waligundua alikuwa amefariki muda mrefu uliopita
Imeelezwa kuwa mume wa marehemu alisisitiza kuwa mke wake hajafa bali amezimia kwa muda mrefu
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha , Charles Mkumbo alithibitisha tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na kifo hicho cha maombi tatanishi
Chanzo :HabariLeo