Police kusini mwa Hyderabad wameimbia BBC wanachunguza iwapo Aradhana Samdariya alilazimishwa kufunga.
Wazazi wake wanasisitiza kuwa alifunga kwa hiari kama inavyotakiwa katika Jainism, mojawapo ya dini za jadi duniani.
Mkasa huo umesababisha mjadala kuhusu ibada ya kufunga India.
Ripoti zinasema Aradhana alikunywa maji ya kuchemshwa tu kwa siku 68.
Siku mbili baada ya kusitisha kufunga wiki iliyopita, alifariki.
Wataalamu wanaamini binaadamu anaweza kukaa bila ya chakula kwa hadi miezi miwili.
Msemaji wa polisi amesema kesi imeanzishwa dhidi ya wazazi wa mtoto huyo baada ya shirika la kutetea haki za watoto kuwasilisha malalamiko.
Kufunga kwa hiari?
"Wazazi wake - LaxmiChand na Manshi Samdariya - wameshtakiwa kwa kutekeleza mauaji kwa kupuuza na kwa kukiuka sheria ya watoto," msemaji alisema.
Wazazi hao ambao ni watengenezaji vyombo vya thamani vya mapambo ya mwili, wamekana kuwa walimlazimisha binti yao kufunga.
"Aliomba ruhusa kufunga upvaas. Tulimwambia akatize baada ya siku 51 lakini alikataa. Alifunga kwa hiari, hakuna aliyemlazimisha," Bwana Samdariya alisema.
Lakini wanaharakati wa kijamii wamepinga tuhuma ya wazazi hao.
Kifo cha msichana huyo kwa mara nyingine kimeangazia kuhusu ibada na tamaduni kama hizo.
Kufunga ni kawaida kwa baadhi ya dini - Waislamu hufunga kula na kunywa kuanzia jua linapopaa mpaka linapotuwa wakati wa mwezi wa Ramadhani, Wakristo hufunga wakati wa Lent, Wayahudi hufunga kula wakati wa Yom Kippur na Wahindu hufunga wakati wa shughuli mbalimbali za kidini.
Lakini dini zote hazikubali kufunga kiasi cha mtu kufa na njaa.
Hatahivyo, viongozi wa dini ya Jain wametetea kufunga kwa muda mrefu.
Source: BBC