Mwanamuziki wa nyimbo za injili Tanzania John Lisu amezindua album yake mpya inayoitwa Mtakatifu worthy of our worship jumapili ya October 2, 2016 katika ukumbi wa kanisa la City Christian Center Upanga na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji la Dar.
Katika Uzinduzi huo John Lisu alisindikizwa na wanamuziki mbalimbali wa nyimbo za injili toka Tanzania na Kenya, ambapo kutoka Tanzania alisindikizwa na Samuel Yonah, Bomby Johnson, Angel Benard, Abenego and the Worshipers toka Arusha, na Mshindi wa GSS mwaka 2016 Sulleiman Wilson. toka Kenya akisindikizwa na mwanamuziki Mercy Masika
Album hii iliwekwa wakfu na wachungaji wa John Lisu toka kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church DPC lililopo Kinondoni Manyanya Dar ambapo Mchungaji kiongozi Dr. Abel Majaliwa na Mch. Mwende waliwaongoza watu mbalimbali waliohudhuria kuiombea album hiyo ikafanye kile ilikusudiwa kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa watu mbalimbali kwa njia ya nyimbo.
Katika kuinadi album hiyo rasmi, Kiasi cha Pesa ikiwa ni ahadi zaid ya Sh16milion zilipatikana katika harambee iliyofanyika kwa kuiuza album hiyo ukumbini.
Wakati uzinduzi huo ukielekea ukingoni Mc wa shughuli hiyo Fred Msungu alimsimamisha ukumbini kwa suprize Mwanamuziki wa Bongo Flava Peter Msechu ambaye aligeuka kuwa kivutio kwa watu waliohudhuria shughuli hiyo pale ambapo Mc alimtaka kutoa ahadi naye atatoa shiling ngapi kuinunua album hiyo ya Lisu.
Peter Msechu aliwashangaza watu kwa aina ya ujibuji swali hilo kwa kuanza kutoa maelezo kuwa amekuwa karibu na timu nzima ya wanamuziki na waimbaji pamoja na John Lisu wakati wakiandaa album hii na mara kwa mara alikua akiwatembelea studioni aliwakuta wakiwa wanapiga mazoezi ya kurekodi huku mifuko yao ikiwa imetoboka.
"Nilikua nikiwakuta sometime wanaimba wanapiga mziki lakini unakuta hawana hata hela ya chips hivyo jamani hebu tufanye jambo hapa ili kuwapiga tafu kidogo" alisema Msechu
Mwisho Msechu alisema kuwa yeye hana hata sh mia mfukoni ila sadaka yake kwa John Lisu ni Kuimba wimbo wa Yu hai Jehova na watu waliohudhuria ukumbini watoe hela ya kumtuza ambapo hela hiyo atamkabidhi Lisu, na kutishia kuwa ambaye hatatoa basi asishangae shetani atakapoziiba hizo hela na kuwaacha wakiwa tupu.
Mwitikio ulikua mkubwa ambapo wakati Msechu alipoanza kuimba wimbo huo kundi kubwa la watu lilijitokeza na kuanza kumtuza kwa fedha, na baadae alizikabidhi kwa John Lisu na waandaaji wa shughuli hiyo, kisha Mc Fred Msungu na waumini wakafanya Maombi mazito kumuombea Msechu arudi kwenye mziki wa injili na kutoka kwenye Bongo Flava.