Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.
''Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku'' Amesema Waziri Majaliwa.
Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.