Katika ulimwengu huu wa digitali kumekua na mitandao mingi ya kijamii ikiwa ni pamoja na facebook,Twitter,Instagram na mitandao mingine mingi ya kijamii inayowaunganisha watu pamoja kujadili na na kushirikishana masuala mbalimbali ya kijamii..
katika kuendana na ulimwengu wa digitali ,Kundi moja la Kikristo nchini Ghana linapanga kuzindua mtandao wa kijamii ambao unaelezwa kuwa 'mtakatifu'.
Kundi hilo la Love Realm linasema mtandao huo hautakuwa na habari, picha, sauti au hata video zenye ujumbe unaoenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kikristo.
Viongozi wa kundi hilo wanasema mitandao ya sasa ya kijamii imejaa picha, video na habari zenye maudhui ya utupu na ukatili.
Lakini kundi hilo, lililoanzishwa na Dkt Yaw Ansong Jnr na Bojan Jordanovski, limejinasibu kuwa mtandao wao ujao utawasaidia wale ambao walikuwa na mahangaiko ya kulinda imani zao dhidi ya mitandao isiyokuwa na maadili na mtandao huo pia utasaidia washirika wake kuungama na kutubu dhambi.
Kwa sasa mtandao huo umekwisha waalika maelfu ya wafuatiliaji Wakristo wafanye majaribio ya kushiriki katika tovuti hiyo katika kituo cha Pentekoste katika mji mkuu, Accra.