Waziri Mkuu wa zamani Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na Waziri Mkuu wa sasa Mhe.Kassim Majaliwa walipokutana leo kwenye ibada ya kumuapisha Askofu Dr.Fredrick Shoo kuwa Mkuu mpya wa Kanisa la KKKT. Ibada hiyo imefanyika Kanisa la KKKT Moshi mjini.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Jumapili hii 31January linaandika historia baada ya kuapishwa kwa Akofu Dr.Fredrick Shoo kuwa Mkuu Mpya wa Kanisa hilo katika ibada inayofanyika Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini.
Ibada hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ambaye ndiye Mgeni Rasmi, Maaskofu wote wa KKKT Tanzania, baadhi ya maaskofu wa Kanisa Katoliki na makanisa Mengine, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na wageni wengine wa ndani na nje ya nchi.
Askofu Dr.Fredrick Shoo alichaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa la KKKT mwaka jana mwezi August kuchukua nafasi ya Askofu Mkuu Dr.Alex Malasusa anayemaliza muda wake leo.
Dr.Shoo anakuwa Askofu Mkuu wa 5 wa Kanisa hilo akitanguliwa na Askofu Stefano Moshi aliyekuwa Mkuu wa Kwanza wa Kanisa (1963-1976), Askofu Dr.Sebastian Kolowa (1976-1992), Askofu Dr.Samson Mushemba (1992-2007), na Askofu Dr.Alex Malasusa (2007-2016).
Askofu Dr.Shao alizaliwa mwaka 1959 huko Machame mkoani Kilimanjaro na alibarikiwa kuwa mchungaji mwaka 1986 baada ya kuhitimu shaahada yake ya kwanza ya Theolojia chuo cha Makumira (kwa sasa kinaitwa Chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Makumira).
Kati ya mwaka 1988 hadi mwaka 1990 alihitimu Shahada ya uzamili katika Theolojia (Master degree in Theology), na mwaka 1990 alianza masomo yake ya shahada ya uzamivu (PhD) nchini Ujerumani ambapo alihitimu mwaka 1995.
Mwaka mmoja baadae (2004) Dr.Shoo alichaguliwa kuwa Askofu msaidizi wa Dayosisi ya Kaskazini chini ya Askofu Dr.Martin Shao. Mara baada kusimikwa kuwa Askofu Msaidizi tulimwalika kwenye Kongamano la Pasaka (Easter Conference) pale Seminari ya Agape ambapo alitufungulia kongamano hilo.
Dr.Shoo aliendelea kuwa Askofu Msaidizi hadi mwaka 2014 alipochaguliwa kuwa Askofu Kamili wa Dayosisi ya Kaskazini.
Mwaka mmoja tu wa utumishi kama Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, akachaguliwa na Mkutano mkuu wa 19 wa Kanisa hilo kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Askofu Dr.Fredrick Shoo ameoa na ana watoto watatu.
Ni mtu mpole, mnyenyekevu, na mstahimilivu. Humsikiliza kila mtu bila kujali nafasi yako. Ni mtu mwenye maono (Visionary) na mkarimu. Licha ya kwamba ni msomi mzuri (PhD) lakini Hajikwezi kama ilivyo kwa wasomi wengine.
Hongera Askofu Shoo, Hongereni Dayosisi na Kaskazini, Hongereni KKKT kwa kumpata Mkuu mpya wa Kanisa. Hongera pia Watanzania kwani KKKT imekua mdau mkubwa wa maendeleo kwa kumiliki Shule, Vyuo, Hospitali ambavyo vimekuwa vikihudumia watanzania wote bila kujali imani zao.
Source: Malisa GJ