Mgogoro wa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakidaiwa katika madai ya kesi ya haki miliki ya wimbo wenye umaarufu mkubwa duniani wa 'happy birthday' umetatuliwa kabla kesi hiyo haijatolewa hukumu huko Los Angeles nchini Marekani.
Kampuni ya kurekodi muziki ya Warner Chappel, imesema ilinunua haki miliki ya wimbo huo mnamo mwaka 1935, lakini mwanzoni mwa mwaka huu hakimu anayesimamia kesi hii, alisema wimbo huo hauna haki miliki ya kuwa na mashairi yenye lugha ya kiingereza.
Wanamuziki na watengeneza filamu wametakiwa kulipia dola milioni mbili kwa mwaka kama gharama ya kuutumia wimbo huo kwa umma kwa mwaka. Ingawa vigezo vyake bado havijawekwa wazi.
Wanamuziki na watengeneza filamu wametakiwa kulipia dola milioni mbili kwa mwaka kama gharama ya kuutumia wimbo huo kwa umma kwa mwaka. Ingawa vigezo vyake bado havijawekwa wazi.