Mh.John Pombe Joseph Magufuli ameapishwa rasmi siku ya leo November 5,2015 kuwa rais wa awamu ya tano na Amiri jeshi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa na Marais wa nchi mbalimbali za Afrika na Dunia pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.
Rais Magufuli anaanza rasmi Uongozi wake ikiwa pia ni siku ya kustaafu rasmi kwa aliyekua rais wa awamu ya nne wa Mh.Jakaya Mrisho Kikwete.
Picha za tukio zima la Uapishwaji wa rais John Magufuli ni kama zinavyoonekana hapa
Rais John Magufuli akikagua gwaride kwa mara ya kwanza kabisa kama Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Picha za tukio zima la Uapishwaji wa rais John Magufuli ni kama zinavyoonekana hapa
Rais John Magufuli akila Kiapo cha kulitumika taifa la Tanzania kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Rais John Magufuli akisaini Kupokea Uongozi kama Rais wa Tanzania |
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu akila Kiapo cha kulitumikia taifa la Tanzania kama Makamu wa Rais |
Rais John Magufuli akipewa pongezi toka kwa Rais Uhuru Kenyata wa Kenya baada ya kuapishwa |
Rais Magufuli akiwa na Marais mbalimbali wa nchi za Afrika |
Rais John Magufuli akiwa na Rais Uhuru Kenyata na Mh.Raila Odinga |
Wake wa marais wa nchi za Afrika Mashariki |