Kutoka huko Harare Zimbabwe,Nabii mmoja aliyejulikana kama Sham Hungwe kutoka kanisa liitwalo House of Grace International Church Zimbabwe ,amejitokeza na mapya na kuibuka kwenye vyombo vya habari akisema kwamba anauza Peni za upako ambao kila mwanafunzi atakayenunua peni hizo ataweza kufaulu mtihani bila hata kusoma.
Nabii Sham Hungwe |
Kikawaida masuala ya upako,yamekua yakisemwa sana ambapo kumekuwepo na watumishi wakitoa mafuta ya upako,maji ya upako,Vitambaa vya Upako,lakini nabii Sham Hungwe yeye amekuja na aina yake ya Upako ambao katika ibada akiwa na wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya O level na A Level amedai kwamba kiwango cha pesa ambacho mtu anakitoa kununua peni kinalingana na kiwango cha nafasi ya ufaulu ya mwanafunzi kwenye mtihani ambao mwanafunzi atafanya kwa kutumia peni hiyo.
Nabii huyo aliweza kuuza peni nyingi zaidi kwa wanafunzi ambapo peni moja iliuzwa kwa takriban dola za kimarekani kuanzia dola 1 hadi dola 20 kwa peni moja
Mauzo ya peni hizo yaliongezeka kwa wingi zaidi na watu kugombania kuzinunua kwa wingi baada ya Mtu mmoja kutoa ushuhuda kanisa hapo kwamba mwaka uliopita yeye aliweza kupata point 14 za ziada baada ya kutumia peni za nabii huyo kufanyia mtihani wake wa A Level
Hata hivyo Nabii huyo amekabiliwa na Upinzani mkubwa sana toka kwa wanasiasa na waandishi wa habari ambapo baadhi wametaka akamatwe na kuwekwa kizuizini kwa kosa la kuharibu kiwango cha elimu nchini humo huku wengine wakidai kwamba huko ni kumdhihaki Mungu kwa sababu Upako hauwezi kufanywa kua Bidhaa ya kuuzwa na kumchanganya na Roho mtakatifu,huko ni kumfanya Mungu kua kitu chepesi hali ambayo ni Kufuru mbele za Mungu.