“Mimi nimezaliwa Mkoa wa Iringa miaka zaidi ya 40 iliyopita. Nimekulia Iringa. Nimesomea Iringa. Mambo haya ya uchungaji nimeanzia Iringa.Kipindi hicho naanza huduma ya kumtumikia Mungu, wakati huo pale Iringa kulikuwa na makanisa mawili ya Kipentekoste.
Mzee wa Upako Mchungaji Anthony Lusekelo
Moja lilikuwa pale Mwembetogwa la Askofu mstaafu Amulike Mboya na lingine la TAG (Tanzania Assembles of God) pale Kwa-Mkane, kitu kama hicho. Nimesali pale na mmoja wa watu wanaojua historia ya maisha yangu ni Mchungaji Mboya. Mboya ni mzee wa siku nyingi sana pale Iringa.
|
Mzee Mboya alifika Iringa tangu miaka ya 1960. Mzee Mboya hakunifahamu tu baada ya kuokoka lakini Mzee Mboya alikuwa family friend. Alikuwa rafiki wa familia yangu. Anaijua vizuri historia ya familia yangu hata baba yangu.
Hata watoto wake akina nani yule (hakumtaja jina), tulisoma wote. Wakati mimi naokokoka, Kanisa la TAG lilikuwa na mgogoro mkubwa pale Iringa kati ya miaka ya 1970 na 1980. Nilipopata wito wa kumtumikia Mungu, mimi nikaangukia upande wa Moses Kulola (marehemu).
Unajua pale Iringa kulikuwa na upande wa Lazaro na Kulola hivyo mimi nikaangukia kwa Kulola.
Mchungaji wangu alikuwa ni Elia Ngobito. Elia Ngobito ndiye alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa kanisa letu la Assembles. Tangu pale hadi leo nimekuwa nikiendelea na uchungaji.
=ASILI YAKE Asili yetu, mimi na baba yangu ni Wanyakyusa wa Mbeya-Mwakareli huko (wilayani Rungwe). Baba yangu alihamia Iringa mwaka 1958. Wazazi wangu walihama Mwakareli kule Mbeya.
Nafahamu kuongea Kihehe. Lakini nilipapenda zaidi Iringa maana nimezaliwa pale nimekulia pale na nimesoma pale. Hata baba yangu wakati anahama Iringa tena kurudi nyumbani Mbeya mimi nilikataa. Nikabaki Iringa.
=FAMILIA Mimi nimeoa na nina watoto wanne, Mode, Salome, Mishael na Elishadai. (anacheka) hahahahaa…Majina yao yanafanana…. Baada ya kutoka Iringa nilifika hapa Ubungo (Kibangu) mwaka 1992.
Ndiyo nilianza kuwa mchungaji hapa tangu mwaka 1992. Kwa hiyo, sasa nina miaka zaidi ya 20 hapa. Lakini hasa kutoka miaka ile ya 92.
Wakati huo kanisa lilikuwa changa na watu kama 35. Mungu akanipa maono haya ya maombezi, miujiza na ishara, nikaanza kutumia vyombo vya habari, TV, redio na magazeti ndiyo maana huduma imekuwa kubwa kiasi hiki.
=MTAZAMO Ukiniuliza nini mtazamo wangu kuhusu makanisa mengine ya Kikiristo nitakuambia kuwa nayaheshimu sana makanisa mengine.
Hakuna kanisa ambalo halina mchango kwenye Ukristo. Kwa mfano, Kanisa Katoliki wana mchango mkubwa sana kwenye Ukristo