Viongozi wakuu katika serikali ya Zambia wamehudhuria siku kuu ya kitaifa ya kufunga na kuliombea taifa hilo ilikunusuru thamani ya sarafu yake.
Maombi hayo yameitishwa kutokana na mfumuko wa bei ya vyakula na bidhaa nyingine muhimu mbali kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo linalotegemea kwa kiwango kikubwa mauzo yatokanayo na madini ya shaba.
Kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa baa zote na vilabu vya burudani vimefungwa
Thamani ya sarafu ya Zambia, Kwacha, imedorora mno na kupoteza takriban nusu ya thamani yake katika kipindi cha miezi 9 iliyopita.
Kufikia sasa Sarafu hiyo imepoteza asilimia 45% ya thamani yake ikibadilishwa na dola ya Marekani.
Hali hii watafiti wa maswala ya kiuchumi wanasema imetokana na mfumuko wa bei ya shaba ambayo imeanguka mno kufuatia mfumuko katika uchumi wa mteja wake mkuu China.
Rais Edgar Lungu amehutubia taifa hilo wakati wa hafla hiyo kubwa iliyofanyika katika mji mkuu Lusaka.
Rais Edga Lungu ameongoza siku ya maombi ilikunusuru uchumi wa taifa hilo |
Kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa baa zote na vilabu vya burudani vimefungwa
Maombi hayo yameitishwa kutokana na mfumuko wa bei ya vyakula na bidhaa nyingine muhimu mbali kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo |
Na si hayo tu waandalizi wa siku hii maalum ya maombi pia wamehakikisha kuwa hakuna uraibu wowote unaoendelea kwa hata mechi za kandanda ambayo hupendwa sana nchini humo zimeaahirishwa.
Thamani ya sarafu ya Zambia, Kwacha, imedorora mno na kupoteza takriban nusu ya thamani yake katika kipindi cha miezi 9 iliyopita.
Sarafu hiyo imepoteza asilimia 45% ya thamani yake ikibadilishwa na dola ya Marekani. |
Hali hii watafiti wa maswala ya kiuchumi wanasema imetokana na mfumuko wa bei ya shaba ambayo imeanguka mno kufuatia mfumuko katika uchumi wa mteja wake mkuu China.
Rais Edgar Lungu amehutubia taifa hilo wakati wa hafla hiyo kubwa iliyofanyika katika mji mkuu Lusaka.
Mechi za kandanda pia zimeahirishwa |