Hatimaye Kanisa la EAGT City Center Dar es Salaam chini ya Bishop Florian Katunzi lililokua likifanya Ibada zake ndani ya viwanja vya SabaSaba hatimaye waumini wa kanisa hilo na mchungaji kwa ujumla wamefanya maandamano makubwa ya hadhara na kuhama kutoka kwenye Viwanja hivyo vya sabasaba eneo ambalo wamekuwepo kwa takribani miaka mitano 5, na kuhamia kwenye kanisa lao rasmi ambalo lilikua katika Ujenzi wa muda mrefu eneo la Mtoni Mtongani
Ufunguzi huo ulihusisha waumini kuhama na viti vyao kutoka Sabasaba hadi Mtoni eneo ambapo kanisa lipo, na kisha kufunguliwa rasmi na Mchungaji Kiongozi Florian Josephat Katunzi, na kushuhudiwa na wageni mbalimbali waliofanikiwa kufika siku hiyo.
Ibada ya kwanza kanisani hapo itafanyika tarehe 14 Juni, ambapo pia tarehe 5 mwezi Julai ndipo tukio kuu la ibada ya shukurani pamoja na kuwekwa wakfu litafanyika.
Kwa mujibu wa Mchungaji Katunzi eneo hilo jipya lenye
uwezo wa kuchukua takriban waumini 2,500 lina mpango endelevu ambao
utawezesha kuchukua jumla ya waumini 7,200. Na hapo ndipo EAGT City
Centre itadumu na baada ya kufika, hatua inayofata ni kupanuka zaidi.
Sehemu ya umati wa waumini wakitembea kuelekea makao mapya, Mtoni Mtongani kwa Mgaya karibu na daraja la juu la Reli ya Tazara.
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ |