Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Bahati Bukuku amejitokeza rasmi mbele ya uongozi wa chama cha muziki wa injili nchini Tanzania na kutoa taarifa yake rasmi kuamua kusimama pamoja na mmoja kati ya wanaotangaza nia kuwania uraisi nchini Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM,Mh.Edward Lowassa anayetarajia kutangaza nia yake mjini Arusha.
"Bahati Bukuku ametoa taarifa rasmi kwa uongozi wa Chama cha Muziki wa Injili nchini Tanzania CHAMUITA na kubainisha wazi kwamba atakua ni miongoni mwa watu watakao kuwepo mjini Arusha katikaViwanja vya Shekh Amr Abedi kumuunga mkono Mh. Edward Lowasa anapoenda kutangaza nia katika harakati za kusaka Uraisi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Kutoka kushoto ni Rais wa CHAMUITA Addo Novemba, Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Bahati Bukuku, na Katibu Muenezi wa CHAMUITA Stella Joel |
Mmoja wa Viogozi wa chama hicho cha Muziki wa injili Tanzania Katibu Muenezi wa CHAMUITA Stella Joel ameeleza kwamba wao kama viongozi wamemuelewa na wanamtakia kila la heri katika safari yake na shughuli nzima ya kumuunga mkono Mh. Edward Lowasa".