Ni maumivu Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kutoka Hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa kwa siku tano kwa kutumia baiskeli ya wagonjwa (wheelchair) kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kuhojiwa kwa mara ya pili.
Wakati akipelekwa katika gari Askofu Gwajima, alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali ambayo haikujulikana mara moja chanzo chake.
Baada ya wafuasi wake kukamilisha taratibu zote, ilipofika saa 6:15 mchana, gari la polisi aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili KX 06 EFY liliwasili hospitalini hapo.
Gari hilo, lilikuwa na askari wanne, mmoja akiwa ni ofisa wa polisi aliyekuwa amevalia sare za askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
Asakari hao ambao walikuwa wamebeba bunduki walikwenda moja kwa moja wodini na baadae kutoka pamoja na kiongozi huyo wa kiroho.
Baada ya muda kidogo, askari hao walishuka chini na ilipofika saa 06:34 chana, gari nyingine ndogo aina ya Yutong MG 6 Turbo yenye namba STL 110 iliwasili eneo hilo ikiwa na askari mmoja.
Akiwa anainuliwa kwenye kiti na kupandishwa katika gari, Askofu Gwajima alionekana akikunja uso na kufungua mdomo kama mtu anayegugumia kutokana na maumivu makali.
Baada ya kutoka hospitalini, msafara huo ulielekea moja kwa moja
Alipofika mlangoni alikutana na ofisa mmoja, ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja, alimuaru asubiri ili wakili wake afanye taratibu za dhamana.
“Subiri hapa mfanye taratibu za dhamana mkishamaliza hakikisha Alhamisi (kesho) unaripoti Central Polisi (kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam),”alisikika ofisa huyo akisema.
WAFUASI WAKUSANYIKA
Wakati taratibu za dhamana zikiendelea, wafuasi wa Askofu Gwajima waliendelea kukusanyika eneo hilo kwa madai kuwa wanamsubiri kiongozi wao.
Wakiwa wamekusanyika makundi makundi, huku wengine wakiwa wameshikilia makaratasi yenye maandishi na picha ndogo kwa ajili ya kusaidia udhamini kama ukihitajika.
Ilipofika saa 8:00 mchana, gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T 631 AHD iliingia kituoni hapo na muda mfupi ikaondoka na Askofu Gwajima.
Baada ya kuonekana akiwa ndani ya gari hilo, wafuasi wake walianza kushangilia na kuimba “tumeshinda, tumeshinda tumeshinda…yesu, yesu, yesu…”
Gari hiyo, ilizingirwa na wafuasi wake huku waandishi wa habari nao wakitafuta upenyo wa kuzungumza ambapo askofu huyo alitamka maneno machache akisema.
Baada ya kuondoka wafuasi wake walitembea kwa miguu kutoka Oysterbay hadi Kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima, huku wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu.
Naye mwanasheria wa Askofu Gwajima, John Mallya alisema mteja wake ameachiwa kwa dhamana isiyo na masharti.
“Mteja wangu, ameachiwa kwa dhamana isiyo na masharti na tumeamua akapumzike nyumbani kwa kuwa hali yake ya kiafya bado si nzuri,” alisema Mallya.
Awali kabla yakuchukuliwa na polisi hospitalini,daktari aliyekuwa akimtibu, Dk. Fortunatas Mazigo, alisema Askofu Gwajima asingeweza kuruhusiwa kutoka hospitalini jana kwa sababu hali yake haikuwa ya kuridhisha.
“Hatutarajii kumruhusu leo bado hayuko vizuri,endapo atahitajika kuripoti polisi tutampa kibali cha muda na atapaswa kurudi hospitalini kwa sababu hajaweza kutembea, labda kwa msaada wa watu ingawa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa juzi,” alisema Dk. Mazigo.
MAASKOFU WAKUTANA
Katika hatua nyingine, maaskofu na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste walioandamana na viongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, walifika Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa ajili ya kukutana na maofisa wa polisi ili kuzungumzia suala hilo.
Msafara wa viongozi hao, uliongozwa na Mchungaji Samwel
Kikao cha viongozi hao na maofisa wa polisi kilianza saa 4 asubuhi na kilidumu kwa zaidi ya saa moja, huku waumini wengine wakiendelea kusubiri nje.
Hata hivyo, waumini hao walifukuzwa na polisi waliokuwa doria.
Maaskofu walipotoka nje ya kikao hicho, waliwaeleza waumini wao kwamba wanapaswa kwenda kuonana na Mkuu wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Mchungaji Ndege, akiongozana na wenzake saba walifika makao makuu ya polisi saa 7 mchana.
Kikao chao na IGP Mangu kilikuwa cha ndani, huku waandishi wakizuiwa kuingia ndani.
KOVA AZUNGUMZIA
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova alisema Askofu Gwajima pamoja na wafuasi wake 15 wote na upelelezi ukikamilika watafikifishwa mahakamani.
Alisema Askofu Gwajima na wenzake wanayo haki ya kupewa dhamana, ingawa wanatakiwa kurudi kituoni kuripoti kwa tarehe waliyopangiwa.
Askofu Gwajima, alipandishwa kwenye baiskeli hiyo, baada ya kupelekewa na mmoja wa wafuasi ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kichungaji.
Wakati akipelekwa katika gari Askofu Gwajima, alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali ambayo haikujulikana mara moja chanzo chake.
Baada ya wafuasi wake kukamilisha taratibu zote, ilipofika saa 6:15 mchana, gari la polisi aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili KX 06 EFY liliwasili hospitalini hapo.
Gari hilo, lilikuwa na askari wanne, mmoja akiwa ni ofisa wa polisi aliyekuwa amevalia sare za askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
Asakari hao ambao walikuwa wamebeba bunduki walikwenda moja kwa moja wodini na baadae kutoka pamoja na kiongozi huyo wa kiroho.
Baada ya muda kidogo, askari hao walishuka chini na ilipofika saa 06:34 chana, gari nyingine ndogo aina ya Yutong MG 6 Turbo yenye namba STL 110 iliwasili eneo hilo ikiwa na askari mmoja.
Ilipofika saa 6:45, Askofu Gwajima alishushwa katika lifti ya hospitali hiyo, akiwa anasindikizwa na zaidi ya watu wane, huku yeye akiwa amekaa kwenye baiskeli hiyo na kupandishwa moja kwa moja kwenye gari la polisi.
Akiwa anainuliwa kwenye kiti na kupandishwa katika gari, Askofu Gwajima alionekana akikunja uso na kufungua mdomo kama mtu anayegugumia kutokana na maumivu makali.
Baada ya kutoka hospitalini, msafara huo ulielekea moja kwa moja
Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Alifikishwa kituoni hapo saa 6:55 na kupelekwa chumba kilichokuwa kimeandikwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni.
Alifikishwa kituoni hapo saa 6:55 na kupelekwa chumba kilichokuwa kimeandikwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni.
Alipofika mlangoni alikutana na ofisa mmoja, ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja, alimuaru asubiri ili wakili wake afanye taratibu za dhamana.
“Subiri hapa mfanye taratibu za dhamana mkishamaliza hakikisha Alhamisi (kesho) unaripoti Central Polisi (kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam),”alisikika ofisa huyo akisema.
WAFUASI WAKUSANYIKA
Wakati taratibu za dhamana zikiendelea, wafuasi wa Askofu Gwajima waliendelea kukusanyika eneo hilo kwa madai kuwa wanamsubiri kiongozi wao.
Wakiwa wamekusanyika makundi makundi, huku wengine wakiwa wameshikilia makaratasi yenye maandishi na picha ndogo kwa ajili ya kusaidia udhamini kama ukihitajika.
Ilipofika saa 8:00 mchana, gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T 631 AHD iliingia kituoni hapo na muda mfupi ikaondoka na Askofu Gwajima.
Baada ya kuonekana akiwa ndani ya gari hilo, wafuasi wake walianza kushangilia na kuimba “tumeshinda, tumeshinda tumeshinda…yesu, yesu, yesu…”
huku wakiikimbilia gari kwa nyuma na ndipo gari hiyo ilisimama nje kidogo ya kituo hicho.
Gari hiyo, ilizingirwa na wafuasi wake huku waandishi wa habari nao wakitafuta upenyo wa kuzungumza ambapo askofu huyo alitamka maneno machache akisema.
“viongozi wa dini wawe wa kweli na wasimamie ukweli na uwazi daima,” alisema Gwajima.
Baada ya kuondoka wafuasi wake walitembea kwa miguu kutoka Oysterbay hadi Kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima, huku wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu.
Naye mwanasheria wa Askofu Gwajima, John Mallya alisema mteja wake ameachiwa kwa dhamana isiyo na masharti.
“Mteja wangu, ameachiwa kwa dhamana isiyo na masharti na tumeamua akapumzike nyumbani kwa kuwa hali yake ya kiafya bado si nzuri,” alisema Mallya.
Awali kabla yakuchukuliwa na polisi hospitalini,daktari aliyekuwa akimtibu, Dk. Fortunatas Mazigo, alisema Askofu Gwajima asingeweza kuruhusiwa kutoka hospitalini jana kwa sababu hali yake haikuwa ya kuridhisha.
“Hatutarajii kumruhusu leo bado hayuko vizuri,endapo atahitajika kuripoti polisi tutampa kibali cha muda na atapaswa kurudi hospitalini kwa sababu hajaweza kutembea, labda kwa msaada wa watu ingawa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa juzi,” alisema Dk. Mazigo.
MAASKOFU WAKUTANA
Katika hatua nyingine, maaskofu na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste walioandamana na viongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, walifika Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa ajili ya kukutana na maofisa wa polisi ili kuzungumzia suala hilo.
Msafara wa viongozi hao, uliongozwa na Mchungaji Samwel
Ndege wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Kikao cha viongozi hao na maofisa wa polisi kilianza saa 4 asubuhi na kilidumu kwa zaidi ya saa moja, huku waumini wengine wakiendelea kusubiri nje.
Hata hivyo, waumini hao walifukuzwa na polisi waliokuwa doria.
Maaskofu walipotoka nje ya kikao hicho, waliwaeleza waumini wao kwamba wanapaswa kwenda kuonana na Mkuu wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Mchungaji Ndege, akiongozana na wenzake saba walifika makao makuu ya polisi saa 7 mchana.
Kikao chao na IGP Mangu kilikuwa cha ndani, huku waandishi wakizuiwa kuingia ndani.
KOVA AZUNGUMZIA
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova alisema Askofu Gwajima pamoja na wafuasi wake 15 wote na upelelezi ukikamilika watafikifishwa mahakamani.
Alisema Askofu Gwajima na wenzake wanayo haki ya kupewa dhamana, ingawa wanatakiwa kurudi kituoni kuripoti kwa tarehe waliyopangiwa.
Chanzo:Mtanzania