DHAMBI INABOMOA NA KUMONGO'NYOA UTUKUFU WA MUNGU MAISHANI MWAKO.
RUM. 3:23 SUV
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Moja ya uwongo ambao shetani ametuuzia nasi tumeununua kama vipofu ni kwamba sio shida kabisa kufanya dhambi alimradi tunatubu.
Tumedanganywa kwamba Mungu ni wa huruma, rehema na neema na kwa sababu hiyo tukitenda dhambi tukamwendea atatusamehe.
Moja ya vitu ambavyo shetani hataki tuone kama athari za dhambi maishani mwetu ni kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Utukufu wa Mungu ni uwepo wa Mungu uliyodhihirishwa.
Dhambi inaporuhusiwa kuingia maishani mwetu athari zake ni zaidi ya kuvuruga uhusiano wetu na Mungu. Dhambi inaathiri utukufu wa Mungu juu yetu. Uwepo wa Mungu uliyodhihirishwa maishani mwetu unapungua na kwa kadiri dhambi inavyoendelea kuachwa maishani mwetu inaendelea kumong'onyoa Utukufu wa Mungu juu yetu.
Kwa kadiri dhambi inavyoendelea maishani mwetu inaupunguza uwepo wa Mungu uliyodhihirishwa maishani mwetu.
Huwezi ukatamani kutembea na Uwepo wa Mungu maishani mwako na wakati huo huo unacheza na dhambi.
Dhambi inamong'onyoa Utukufu wa Mungu katika maisha yetu.
Hata ukitubu, ni kweli utasamehewa ila ndo kuna kiwango cha Utukufu wa Mungu kitakuwa kimepunguzwa na utahitaji kujengwa tena.
Sasa kama ni maisha ya dhambi kutubu, dhambi kutubu japo toba yako itakupatia msamaha lakini Uwepo wa Mungu unaojidhihirisha maishani mwako utapata athari kubwa.
Wana wa Israeli walikuwa wanatembea na Mungu katika safari yao ya toka Misri kwenda nchi ya Kaanani. Walipomkosea Mungu mara kwa mara Mungu akasema hataenda nao tena asije akawaangamiza akasema atawatumia Malaika aende nao. Hii ilikuwa punguzo kubwa sana la Uwepo wa Mungu uliyodhihirishwa.
Maisha ya dhambi kwa mtoto wa Mungu inapunguza sana Uwepo wa Mungu uliyodhihirishwa maishani mwake.
Kiu tuliyo nayo ya kuwa na Mungu maishani mwetu lazima iwe sambamba na kiu ya haki na utakatifu.
Na ninaposema Mungu namaanisha Uwepo Wake unaojidhihirisha pamoja nasi maana anaweza akawepo na mtu pasipo kiulazima kuudhihirisha Uwepo Wake au kwa maneno mengine kuwafanya watu wajue kuwa yupo pamoja na wewe.
Yesu alisema maneno haya:
YN. 14:21 SUV
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Kama tunatamani Yesu ajidhihirishe kwetu itatugharimu kuishi maidha ya utakaso, maisha yaliyojitenga na dhambi. Hatuwezintu tukajiishia tu alafu tutegemee Yesu ajidhihirishe kwetu.
Sisi Kanisa tubwazuri sana kupotezea. Tunaweza kutoa kila sababu kwanini Mungu hajidhihirishi leo.
Tunaweza kutoa kila sababu kwanini vipofu hawaoni, viziwi hawasikii, mabubu hawaongei, wagonjwa hawaponi, waliyofungwa hawafunguliwi na kwanini ishara, miujiza na maajabu havionekani.
Lakini ukweli utabaki pale pale. Dhambi imeruhusiwa kuingia na hiyo dhambi imefukuza na kukimbiza Uwepo wa Mungu ukiyodhihirishwa.
Ili Mungu arejee katika Utukufu Wake na Ukuu na Uweza Wake lazima dhambi iende. Dhambi iondoke.
Mtume Yakobo aliandika maneno haya nami nanukuu:
YAK. 4:8-10 SUV
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Gharama ya kumkaribia Mungu Naye akukaribie ni kuishi maisha ya utakaso au ya kujitenga na dhambi. Tusiwe watu wa nia mbili. Tusiwe kwa Bwana alafu bado tunacheza na dhambi alafu wakati huo huo tunataka Bwana awe karibu nasi na wakati huo huo tunataka udhihirisho wa Kimungu pamoja nasi. Tuamue moja kama ni haki ndo inafaa kutumikiwa au dhambi. Tunyenyekee mbele Zake, tujishushe na kujidhili ili atuinue.
Hii itabaki kuwa kweli isiyobatilika:
EBR. 12:14 SUV
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Kama tunataka kumwona Bwana dhambi lazima iondoke katikati yetu.
Tusikubali kuendelea kuununua uwongo wa shetani wa tenda dhambi alafu utatubu maana ndiyo utatubu ila ndo utakuwa ushapoteza kiwango cha Uwepo wa Mungu uliyodhihirishwa maishani mwako na ukiwa mkweli unajua dhambi inavyo athiri ushirika wako na Mungu. Itaiba maisha yako ya maombi. Itabomoa maisha yako ya usomaji na kuliishi neno. Itakuibia mengi.
Dhambi haiwezi ikaruhusiwa mahali alafu isiingie na mshahara wake yaani mauti.
Ukishairuhusu dhambi ujue umeruhusu mauti na hiyo mauti itaanza kuua vitu vya thamani maishani mwako kwa habari ya uhusiano wako na Mungu na kutembea kwako na Mungu.
Amua leo kufukuza dhambi maishani mwako na kutocheza nayo.
Ukicheza na mnyama hatari hata kama ni rafiki kiasi gani kuna siku atakuchenjia.
Dhambi itakuchenjia. Iondoe maishani mwako hasa kama unatamani kutembea na Mungu kiwango kingine.
2 NYA. 7:14 SUV
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
ISA. 55:6-7 SUV
Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Asomaye na afahamu.
na Manna Tabernacle Bible Church.