Wapenzi walimwengu, kiongozi huutumia muda, akili, maarifa, nguvu na ujuzi wake wote ili kulitumikia kundi.
Pili, unyenyekevu hudhihirishwa na utayari wa kupokea mafundisho na maonyo. Nitarejea tena katika hekima za Mfalme Sulemani (Ni kisima cha hekima kwa kila kiongozi)…
Mwandishi James Kalekwa
Hufurahia mafanikio na ustawi wa kundi, na huumizwa na kundi linapodhoofu na kushindwa.
Je, hali ndivyo ilivyo katika nyanja zote za kimaisha huko tuliko? Au ndicho ambacho huwa tunakitafuta pindi tunaposema twahitaji kiongozi? Labda niseme kwa uwazi kidogo, mtu anaye tafuta heshima, utajiri, sifa na mengineyo kupitia nafasi ya uongozi huyo si mtumishi/mtumwa huyo ni bwana mkubwa, ni mchungaji wa mshahara!
|
Pili, unyenyekevu hudhihirishwa na utayari wa kupokea mafundisho na maonyo. Nitarejea tena katika hekima za Mfalme Sulemani (Ni kisima cha hekima kwa kila kiongozi)…
“Kila apendaye mafundisho (instructions), hupenda maarifa; bali achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.”.
Walimwengu, naamini sote twajua kwamba kama tunatafuta kiongozi aliye mkamilifu katika ufahamu wa mambo yooote, basi tunanamtafuta Mungu. Kwani ndiye twaelezwa na wanatheolojia kwamba yeye ni Omniscient (mwenye ufahamu wote).
Lakini katikati yetu wanadamu, naomba tuelewe ya kwamba Hakuna na kamwe hatotokea mtu anayefahamu mambo yote.
Kwa kusema hivyo, mtu yeyote na hasa kiongozi anapaswa si kuwa na moyo wa utayari kuwasikiliza watu wengine (si kusikiliza ili ajibu au apinge) na usikivu huo uwe umejengwa katika misingi ya heshima kwamba anao wasikiliza ni watu wenye ufahamu juu ya jambo fulani, huenda kuliko hata yeye kiongozi.

Mafundisho, maelekezo, maonyo ni muhimu kwa kiongozi! Kila niisomapo ile sehemu ya pili ya mithali ya Mfalme Sulemani ya kwamba “… bali achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.” huwa ninajisikia na ninawiwa kunyenyekea zaidi.
Pia huwa ninainua macho yangu na kuanza kuhesabu ni wanyama wangapi ninaoishi nao katika jamii yangu ambao huwa na mwonekano wa binadamu.
Najua wengi wakisoma huanza kujenga picha ya viongozi wa kisiasa, hapana! Anza na nafsi yako, kaya/familia, ukoo, mtaa, kata, sehemu yako ya kazi, katika nyumba za ibada, taasisi za kielimu n.k kote huko kunahitaji viongozi na si wanyama! Sizuii kuutanua wigo mpaka kwa “viongozi” wa kisiasa na “viongozi” wa nchi… ni ruksa kukagua wanyama wangapi tunao huko pia!
Limezuka wimbi kubwa sasa kwa wasomi wengi kuamini kwa kujidanganya kwamba wao wanayo majibu ya matatizo yote. Hili kundi la wasomi technocrats huzitazama jamii, kwa mitazamo yao ya kisomi, na kuziona zina matatizo chungu mbovu kisha kuziundia suluhisho (ama la muda au la kudumu) pasi na kushirikisha wanajamii husika.

Kwa mara kadhaa nimeshuhudia miradi mingi ikitengenezwa katika meza ya majadiliano na kisha kuweka vipaumbele na utekelezaji wa miradi hiyo huanza.
Punde si punde, kifo cha miradi hiyo hutokea baada ya kipindi cha mradi kwisha. Wakati fulani nilitembelea kata fulani, wilaya moja ya mkoa wa Mara kwa shughuli za kujifunza na utafiti na katika mazungumzo ya hapa na pale na wanajamii. Niligundua kwamba wanajamii hujua vyema matatizo yao na huweza kuainisha vipaumbele vyao na hutekeleza kwa furaha maamuzi yao.
Mradi mmoja uliokuwepo eneo hilo, ulikuwa ni kipaumbele cha nne cha wananchi hao na hivyo walisusia kushiriki katika utekelezaji... Kiongozi huwa na moyo wa utayari kujifunza na kuelekezwa na watu wengine!
Hitimisho:
Binafsi, Napenda kumshukuru mpuuzi Masoud Kipanya kunipa mwanga kupitia upuuzi wake. Nami ninaamini kwamba siwezi kuwa mjuzi wa mambo yote, la sivyo natafuta kuwa Mungu, hivyo kuna watu wengine wanaweza kutoa mwanga zaidi juu ya swala la Uongozi na hatma ya ulimwengu na jamii yetu.
Kwangu huu waweza kuwa mwisho wa mwanzo wa waraka wangu wa kwanza juu ya maswala ya uongozi hasa jamii niishio inapoanza kuzungumza juu ya mwaka 2015!
Kila asomaye na afahamu na kila aonaye ainue kichwa chake na kuchangamka!
Ndimi,
Mtumwa J.K

Mwisho wa mfululizo wa somo hili la Uongozi kutoka kwenye Mambo ya Kipuuzi . Ungana na blog hii jumatano ijayo kwa somo jingine jipya ambalo litaanza kwa mara ya kwanza kabisa.