Walimwengu muishio Tanzania nadhani mmeshawahi kusikia juu ya Vision 2025 (wengi najua bado hawajasikia), MKUKUTA na MKUZA [umahalishaji (contexualization) wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia], Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano, Ilani ya Chama Tawala na Ahadi za Raisi…
Mwandishi James Kalekwa |
Yote hayo ni “maono” ya nchi hii! Yote yanahitaji kufanywa kuwa halisi ndani ya muda usiozidi miaka 13 ijayo!
Je, malengo/maono hayo yanajengana (complementary), yanaingiliana (overlapping) ama yanakinzana (Opposing)? Yanatekelezeka?
Mwl. J.K, rais wa kwanza na baba wa taifa la Tanzania kwa kushirikiana na viongozi wengine waliweka kwanza falsafa ya taifa
Mwl. J.K, rais wa kwanza na baba wa taifa la Tanzania kwa kushirikiana na viongozi wengine waliweka kwanza falsafa ya taifa
“Ujamaa na Kujitegemea.” Na kutoka katika hiyo kuanza kuzaa malengo kufikia huko. Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania 1977 imetanabaisha juu ya hilo na Azimio la Arusha kwa kinagaubaga limeonyesha njia.
Hivyo ni rahisi kuelewa kuwa mipango yote ya nchi ilijengwa juu ya msingi huo! Mwl. J.K akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mwaka 1995 aligusia juu ya jinsi “viongozi” walivyoyaasi maono ya nchi na kuyazika ndani ya Azimio la Zanzibar…
Ndiyo, ndivyo ilivyo! Kwani “malengo” tuliyonayo kama taifa (nimekwisha kuyaainisha hapo juu) yanatuelekeza kwenye falsafa yoyote ya kitaifa (nachelea kusema hatuna falsafa ya kitaifa).
Falsafa ni msingi na malengo ni boma; Sasa sis sijui twajenga hewani? Aaaah! Nimeikumbuka methali isemayo what is the use of running if we are not on the right road. Nami nawaulizeni walimwengu kuna umuhimu gani wa kukimbia kama hatupo kwenye njia sahihi?
Hekima za Mfalme Sulemaini zinatuelekeza kwamba maono hubadili mwenendo na tabia ya mtu kuyaelekea maono hayo. Kama “kiongozi” haishi kuyaelekea maono husika uwe na uhakika kwamba hayaamini maono hayo na hivyo yeye pia ni kipofu.

Kama “maono/malengo” hayamshawishi kiongozi kwenda mwisho wa safari hiyo, hawezi kuwashawishi wanajamii kwenda naye katika mwisho huo! Je, umewahi kuwasikia “viongozi” wakilalamika juu ya maono/malengo kwamba si yao ama hawakuyaweka wao nao walipewa tu kutekeleza?
Binafsi nimeona wataalam wengi wakiangalizia malengo/maono na jinsi ya kuyatekeleza kutoka kwa jamii zingine. Ni vyema kujifunza watu wengine wanafanya nini juu ya mambo fulani lakini siyo kunakili na kuhamishia kwako “Copy and Paste Syndrome”.
Naomba kusisitiza kwenu walimwengu kwamba maono/malengo si tu kuandika juu ya yatakayotokea baada ya muda fulani kisha muda ukifika kuandika taarifa juu ya yaliyotokea.

“Kiongozi” mwenye maono/malengo huwa na mzigo wa kuifikisha jamii yake mahali fulani. Unamkumbuka mwanaharakati na mpigania haki dhidi ya ubaguzi nchini Marekani Dr. Martin Luther King Jr? Umewahi kusikia juu ya baba wa taifa la India, Mahatma Gadhi? Umewahi kujifunza juu ya maisha ya Mwl. J.K na Nelson Madiba Mandela?
Unadhani nini kiliwafanya waishi maisha ya “shida” waliyoyaishi? Unadhani ni kwanini walishikilia na kuweka bidii juu ya waliyokuwa wakiyatafuta? Unadhani ni kwanini watu waliwafuata na kuwaamini? Kwasababu waliokuwa na MAONO/MALENGO waliyoyaona kwa macho yao ya ndani na kuyaamini na kisha kuwashawishi watu kuenda nao katika HATMA hizo huku wakiongoza njia!Na ni kweli walizifikisha jamii zao husika katika nchi ya ahadi. Kila mwenye masikio na asikie.
Mzee Abraham Lincolin aliwahi kusema kwamba kama unataka kujua tabia ya mtu, basi mpatie nafasi ya madaraka/mamlaka.

Karl Max na Marx Weber katika nadharia yao ya Migogoro (Conflict Theory) wanaitazama jamii kama sehemu yenye matabaka na katika matabaka hayo kuna nafasi (positions) ambazo zina viwango tofauti vya mamlaka/madaraka (authority) yaani uwezo wa kutumia/kuonyesha nguvu juu ya watu wengine.
Hivyo jamii ipo katika migogoro endelevu kwakuwa walio katika nafasi za chini wanataka kwenda nafasi za juu na walio nafasi za juu wanataka kulinda nafasi zao ama kwenda juu zaidi. Sivyo ilivyo kwa kiongozi… Kiongozi ni mnyenyekevu!
Nimechagua kuanza maelezo juu ya tabia ya unyenyekevu kwa kueleza walau machache juu ya nadharia ya migogoro ili kusudi nitakapoanza kueleza juu ya unyenyekevu uweze kuchora mstari utenganishao uongozi na u bwana mkubwa!
Unyenyekevu ninaouzungumza hapa ni ule utokanao na neno la kiingereza humility lenye maana ya tabia ya kutojiinua ama kujiona/kujidhani kuwa wewe ni bora kuliko watu wengine. Mimi ni wa thamani kama wewe ulivyo wa thamani. Sote ni binadamu lakini tuna tofauti nyingi sana nazo ndiyo zinatufanya tuhitajiane.

Mimi si kila kitu mpaka uwepo wewe, yule na wale! Ninakuhitaji ndugu msomaji wangu, ninakuhitaji sana! Tofauti iliyomo ndani ya mwanaume na mwanamke kimaumbile, kisaikolojia (tofauti ya tuwazavyo) na kadha wa kadha ni ishara kwamba tunahitajiana! Tunahitajiana ili tuweze kukamilishana … tuunde kitu kamili!
Kiongozi ni mtu ambaye kwa dhati ya moyo wake hutambua na huamini ya kwamba yeye si mkamilifu, si tu kwa maana ya udhaifu, bali kwa kutambua kwamba kuna watu wengine wenye vipaji na ujuzi mbalimbali ambao anawahitaji ili kuwa na kitu kamilifu. Utambuzi huo hudhihirika katika matendo na mwenendo wa kiongozi husika!
Kuna viashiria ambavyo kwavyo hudhihirishwa tabia ya unyenyekevu. Mosi, utumishi/utumwa, hapa ninamaanisha kuchukua wajibu na jukumu la kufanya kazi kwaajili ya jamii fulani na kwa ustawi wa jamii hiyo. Kuwa tayari kuhatarisha mambo yako binafsi kwaajili ya faida ya jamii husika.

Walimwengu, mwaikumbuka hadithi ya mchungaji mwema na mchungaji wa mshahara? Nadhani ni mfano mzuri kuyaeleza haya. Mchungaji wa mshahara huwa na lengo moja kichwani mwake nalo ni kupata mshara, hivyo atatenda yote awezayo ili mwisho apate mshahara.
Twaweza kusema kiu ya moyo wake (passion/zeal) imeelekezwa kwenye mshahara/ujira (Sawa na wale ndugu wawili kati ya watatu kwenye upuuzi wa Masoud Kipanya). Sivyo alivyo mchungaji mwema, yeye hufanya kazi kwa ustawi (welfare) wa kundi la kondoo wake. Kiu ya moyo wake ni kuona kundi lake linaongezeka, lina afya, na lina kuwa tofauti na makundi ya watu wengine.
Huyu hisia zake huguswa na matatizo ya kundi lake. Yuko tayari kudondosha mpaka tone la mwisho la damu na jasho lake kulilinda kundi. Wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala…. Yule wa mshahara akiona mambo hayalipi anatafuta kundi jingine ili mkono uende kinywani. Kwa maneno rahisi, anatafuta nafasi atumie wala si ili atumike!..
itaendelea jumatano ijayo...usikose