Tanzania imekubali kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia kama sehemu ya jitihada zake kusaidia amani na usalama nchini Somalia, lakini baadhi ya maofisa wa Tanzania wameelezea wasiwasi kwamba kujihusisha zaidi katika masuala ya Somalia kunaweza kukaribisha mashambulio ya kigaidi kutoka kwa al-Shabaab.
Mapatano ya kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia 1,000 kwanza yalitolewa mwaka 2012, wakati Tanzania ilipokubali ombi la aliyekuwa rais wa Somalia Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambalo tena limerudiwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud mwaka huu.
"Tumeandaa makambi ya mafunzo na wakati huu ninapozungumza kila kitu kiko tayari. Tunasubiri kutoka kwao kuteua askari 1,000 kuja hapa kwa ajili ya mafunzo,"
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Hussein Mwinyi alisema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) limekuwa likiongoza katika kutoa mafunzo na operesheni za kulinda amani katika Afrika Mashariki na zaidi ya hapo kujenga ushirikiano imara wa kanda.
"Kujenga ushirikiano wa kanda wenye nguvu, TPDF ilifanya mafunzo kadhaa ya kijeshi kwa maofisa wa jeshi na vikosi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika," alisema wakati akihutubia bunge tarehe 21 Mei.
Mwaka uliopita, alisema TPDF ilitoa fursa za mafunzo kwa vikosi na maofisa wa jeshi kutoka Botswana, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Namibia, the Ushelisheli, Swaziland na Zimbabwe.
Pia alisema Tanzania awali iliwahi kutoa mafunzo kwa vikosi vya Somalia katika kutoa mwitiko wa ombi la Umoja wa Afrika, lakini hakusema ni vikosi vingapi vilipewa mafunzo au ni wakati gani.
Alitaja operesheni nyingine ambazo Tanzania ilikuwa na jukumu la kuongoza katika misheni ya kulinda amani ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Lebanon na Sudani ya Kusini.
'Tatizo kubwa' kwa Tanzania?
Wakati serikali iliposema imejiandaa kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia nchini Tanzania, wabunge na raia walitahadharisha dhidi ya kupanua misheni hiyo na kutuma vikosi nchini Somalia.
Job Ndugai, naibu spika wa Bunge la Tanzania, alisema ilikuwa ni hatari kubwa kwa usalama wa taifa kutuma vikosi nchini Somalia, ambavyo vingechochea uhasama wa al-Shabaab.
"Kwa hili nitakuwa mtu wa mwisho kuafiki," Angalia kinachotokea Kenya. Kwa hakika, serikali haipaswi hata kufikiria wazo la kupeleka vikosi nchini Somalia.
"Tumeandaa makambi ya mafunzo na wakati huu ninapozungumza kila kitu kiko tayari. Tunasubiri kutoka kwao kuteua askari 1,000 kuja hapa kwa ajili ya mafunzo,"
alisema Salva Rweyemamu, mkurugenzi wa mawasiliano wa rais wa Tanzania.
"Tunasubiri kuwapa mafunzo kuwa askari wa kitaalamu ili kwamba wadumishe usalama wa nchi yao kutoa fursa ya kujihusisha katika masuala ya maendeleo."
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Hussein Mwinyi alisema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) limekuwa likiongoza katika kutoa mafunzo na operesheni za kulinda amani katika Afrika Mashariki na zaidi ya hapo kujenga ushirikiano imara wa kanda.
"Kujenga ushirikiano wa kanda wenye nguvu, TPDF ilifanya mafunzo kadhaa ya kijeshi kwa maofisa wa jeshi na vikosi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika," alisema wakati akihutubia bunge tarehe 21 Mei.
Mwaka uliopita, alisema TPDF ilitoa fursa za mafunzo kwa vikosi na maofisa wa jeshi kutoka Botswana, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Namibia, the Ushelisheli, Swaziland na Zimbabwe.
Pia alisema Tanzania awali iliwahi kutoa mafunzo kwa vikosi vya Somalia katika kutoa mwitiko wa ombi la Umoja wa Afrika, lakini hakusema ni vikosi vingapi vilipewa mafunzo au ni wakati gani.
Alitaja operesheni nyingine ambazo Tanzania ilikuwa na jukumu la kuongoza katika misheni ya kulinda amani ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Lebanon na Sudani ya Kusini.
'Tatizo kubwa' kwa Tanzania?
Job Ndugai, naibu spika wa Bunge la Tanzania, alisema ilikuwa ni hatari kubwa kwa usalama wa taifa kutuma vikosi nchini Somalia, ambavyo vingechochea uhasama wa al-Shabaab.
"Kwa hili nitakuwa mtu wa mwisho kuafiki," Angalia kinachotokea Kenya. Kwa hakika, serikali haipaswi hata kufikiria wazo la kupeleka vikosi nchini Somalia.
Kama kitatokea chochote, tunapaswa kuwezesha mikutano kwa ajili ya pande zenye migogoro kusuluhisha tofauti zao."
Alisema vikosi vya Tanzania haviwezi kutumwa katika nchi yoyote bila ya ridhaa ya bunge kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama, na ana uhakika kwamba mpango wowote kama huo utazuiwa na wabunge.
"Tanzania haipaswi kujiingiza kabisa katika biashara hii. Nitakuwa mtu wa mwisho kuunga mkono kuingilia kati kwa vikosi kutoka Tanzania kwenda Somalia," Ndugai alisema.
Mbunge Vincent Nyerere, wa chama cha upinzani Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema Tanzania inapaswa kufanya utafiti huru ili kuzingatia kama faida za kujihusisha katika mgogoro wa Somalia zinafaa.
"Tunapaswa kujifunza kutoka kwa ndugu zetu wa Kenya," aliiambia.

"Awali Kenya haikuwa na uhasama na Somalia, lakini kwa kuingilia Somalia wanakabiliwa na mashambulio ya ugaidi mara kwa mara. Tunapaswa kuepuka tatizo hilo."
Deus Kibamba, mkurugenzi mtendaji wa Idara ya Habari kwa Raia wa Tanzania, pia alisema serikali inapaswa kuepuka kujihusisha moja kwa moja katika mgogoro wa Somalia.
Alisema TPDF iliarifiwa kulinda mipaka ya Tanzania na raia wake, lakini mwelekeo wa sasa wa shughuli za amani unampa wasiwasi.
"Vikundi vya magaidi tunavyovisikia kama Boko Haram nchini Nigeria vinafadhiliwa na nchi au watu wenye kinyongo dhidi ya serikali iliyopo madarakani," aliiambia Sabahi. "Kwa kuendelea kusaidia kile tunachokiita uletaji wa amani, polepole tunatengeneza maadui."
"Ninadhani Tanzania hivi karibuni itazitumia rasilimali kupita kiasi kama tutajiingiza katika kila mgogoro unaotokea," alisema. "Tutaanzisha maadui na itakuwa shida kubwa kwa nchi yetu."
Vikosi vya Tanzanian havitapelekwa Somalia
Rweyemamu aliwahakikishia Watanzania kwamba serikali haitapeleka kabisa vikosi nchini Somalia na kwamba "hakujawa na maombi hayo kutoka Somalia wala Umoja wa Afrika".
Rweyemamu pia alitupilia mbali wasiwasi kwamba Tanzania itakuwa ikilengwa na al-Shabaab kwa kuisaidia serikali ya Somalia.
"Kumbukeni kuna serikali kamili nchini Somalia,"

"Tanzania haitakuwa katika ukanda wa vita.
Matakwa yetu, ambayo ni matakwa ya kila mmoja mwenye mawazo kama yetu, ni kuona amani inakuwepo nchini Somalia. Ni katika matakwa ya kila mmoja kurejesha amani nchini Somalia -- iikiwa ni pamoja na al-Shabaab."
Swali: Je, unaunga mkono ushiriki wa Tanzania katika mafunzo ya wanajeshi wa Somalia? Toa maoni yako hapo chini.

source:http://sabahionline.com/